Kufuru, ndege ya watu 150, Malkia wa Nyuki apanda peke yake

Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoosi 'Malkia wa Nyuki'.

MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba watu 150, lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya ndege hiyo.
Rahma, maarufu kama Malkia wa Nyuki, ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320 inayomilikiwa na Serikali ya Oman na anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi wa Heshima wa Oman nchini Morocco.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 17, kati ya hao 16 ni wafanyakazi ndani ya ndege ambao ni daktari mmoja, walinzi wanne, waliobaki ni marubani na wahudumu.
Akizungumza dakika chache kabla ya kuondoka nchini jana, saa 10 alfajiri, Malkia wa Nyuki alisema alishuka nchini kwa ajili ya mapumziko ya siku moja, pia kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba.
“Nimepita tu, tumepumzika kidogo hapa na baada ya hapo ninakwenda Comoro kwa ajili ya kuzungumza na kumchukua Rais wa Comoro.
“Lakini wakati wa mapumziko, nimepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba kuhusiana na mwenendo wa timu kwa hivi sasa.
“Kwa sasa namaliza majukumu yangu kikazi halafu nitarudi tena safari nyingine nchini kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo na viongozi wenzangu wa Simba ili tujue tunaweza kufanya nini kuendelea kurekebisha mambo,” alisema.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Malkia wa Nyuki alisindikizwa na mwanaye Fatma, maarufu kama Nyuki Mtoto na watu wengine wawili.
Baada tu ya yeye kupanda ngazi za ndege hiyo, walinzi na wafanyakazi waliokuwa nje ya ndege hiyo nao waliingia na ikaanza safari kwenda Comoro.CHANZO GPL

Comments

Popular posts from this blog