UNAHISI NI KWANINI HOTUBA YA JK KUMUAGA MANDELA ILIKUWA BORA?
- Get link
- X
- Other Apps
NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .
Nimemwona
na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu
ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela.
Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'.
Hakika
alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa
kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye
uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.
Ni
kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni,
kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari
vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika
harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania
kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama
walivyoonekana kwenye macho ya dunia.
Hakika,
JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena
Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama
na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki
mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata
makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.
JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.
Lakini,
tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni
Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu
ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na
kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.
Na
nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria
ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye
aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru, Thabo
Mbeki baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma
Uingereza.
Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;
" In
1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for
twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he
was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white
Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and
waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle
intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum
in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki
and The Search For Soul of The ANC, pg 36)
Naam, ni
wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa
kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo
huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza
kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali
ya Kimataifa.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment