KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA CHUNYA AJIUNGA NA CCM
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akifafanua jambo wakati alipokuwa
akiuliza swali alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbeya Chunya yenye
kilomita 36 inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 56 za kitanzania ,
Barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kichina ya China Communication
Construction Company, Kinana yuko katika ziara ya kikzani ya mikoa
mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi,
Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa leo amemaliza ziara katika jimbo la Lupa
na kesho anaendelea na ziara katika jombo la Songwe wilayani China,
kulia ni Mh. Abbas Kandoro Mkuu wa mkoa wa Mbeya na katikati ni Dr. Asha
Rose Migiro.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LUPA-CHUNYA)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison
Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya
aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi
CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison
Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya
alikionyesha kadi yake ya chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukabidhiwa
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa.
Mbunge wa
jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh Philip
Mulugo akimvisha shati la CCM Bw. Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya aliporejesha kadi yake ya
chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa
hadhara kata ya Lupa.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akimuangalia Bw. Braison
Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya
wakati akihutubia aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na
chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara kata ya Lupa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa kikundi cha Power Group.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa kikundi cha Nguvu kazi.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa Tingatinga leo.
Kutoka
kulia ni Naibu waziri wa Elimu na Mbunge wa jimbo la Songwe Philip
Mulugo, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki na Nape Nnauye Katibu wa
NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakielekea katika eneo la Mkutano
uliofanyika Kata ya Lupa Chunya.
Baadhi ya wachimaji wadogo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao.
Mkurugenzi
wa Kituo cha mafunzo kwa vitendo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu
Matundasi RSM Development Company Limited Chunya Paul Gongo kulia
akizungumza na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa
Kiamataifa wakati kinana na ujumbe wake walipkagua shughuli za kituo
hicho.
Wachimaji wadogo wakimsikiliza Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo
cha mafunzo kwa vitendo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu Matundasi
RSM Development Company Limited Chunya Paul Gongo wakati alipokagua
shughuli za kituo hicho wilayani chunya leo.
Wananchi
wa mjini Chunya wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana hayupo pichani wakati alipozungumza nao mara baada ya kuwasili
wilayani humo leo.
Msafara wa Kinana ukielekea Chunya
Mkuu wa
wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro akizungumza na wananchi katika
kijiji cha Chalangwa wakati wa mapokezi ya katibu mkuu wa CCM.
Mkurugenzi
wa mtandao wa Fullshangwe Bwana John Bukuku akionyesha moja ya maeneo
yaliyokuwa korofi katika milima ya Kawetere mkoani Mbeya katika barabara
inayotoka Mbeya kwenda Chunya ambayo inaendelea na ujenzi
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment