"BREAKING NEWZ"MATUKIO YA HIVI PUNDE KUTOKA WESTGATE NAIROBI KENYA
Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate...
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa
14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa
14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili
14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi walioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao
13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa
SOURCE BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment