NATAKA KUPATA MTOTO MWINGINE HARAKA ILI BAADA YA HAPO NIJIKITE ZAIDI KATIKA FILAMU - DAVINA


Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Halima Yahaya(Davina) amesema kuwa anataka kupata mtoto mwingine haraka kabla ya aliyemzaa miezi ya karibuni hajawa mkubwa  ili amalizane na kazi ya ulezi na ajikite zaidi katika kazi zake za filamu. "unajua nimeona kuwa kulea siyo kitu cha muda mchache hivyo unatakiwa umalize kwanza ndiyo uendelee na kazi zako ambapo nimeona ni bora nitafute mwingine haraka haraka ndipo nijikite katika filamu" alisema Davina akizungumza na Globalpublishers.

Davina ameigiza filamu nyingi na hivi karibuni filamu yake mpya ya Sababu Ya Nasra akiwa na Slim Omar iliingia sokoni na kwasasa yupo location akishuti filamu mpya na King Majuto, Jenifer Kyaka(Odama) na Rachel Haule.

 Davina

Comments

Popular posts from this blog