Posts

MAJALIWA AMTEMBELEA MALECELA DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. baada ya kuzungumza naye (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph M

STAA WEMA SEPETU ATAJWA KWENYE LIST YA MADAWA YA KULEVYA

Image
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametajwa kuwa ni kati ya wasanii ambao wanatumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kesho kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda katika kituo cha polisi. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amewataja wasanii wengine akiwepo TID, Chid Benz, pamoja na Recho na kusema anahitaji kesho wafike makao makuu ya kituo cha polisi. "Naomba tukutane kesho pale polisi Central akiwepo TID, akiwemo Wema Sepetu, wakiwepo wakina Junior Sniper, wakina Ditto, Titoo, kuna Ally Denya, kuna wakina Chacha, kuna kina Mecky wengine hawa wakina Petit Man tayari nishawatia mikononi mwa sheria, kuna watu kama kina Recho, Chid Benz wote hawa nawahitaji ni vijana wenzangu nafikiri tutaelewana vizuri" alisema Paul Makonda

MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BUNGENI MJINI DODOMA

Image
    Waziri wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana. Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria Februari Mosi, Mjini Dodoma.   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kutetea na kufafa

UFAULU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016 WAPAA

Image
  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016. Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26. Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015. Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.

BREAKING NEWS : ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

Image
THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA. English ... NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania. BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YOTE HAPA

BREAKING NEWZZ:MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA

Image
Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi. Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri. Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea

FARU FAUSTA WA NGORONGORO,ATIMIZA MIAKA 54 AISHI CHINI YA ULINZI WA KIJESHI

Image
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba. Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua hatua juu ya Faru Fausta

BREAKING NEWZZZZ…TRENI YA ABIRIA ITOKAYO KIGOMA KWENDA DAR YADONDOKA

Image
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani leo jioni Jumapili Januari 29, 2017. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa. Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo unmeaning na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio. “Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo