MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BUNGENI MJINI DODOMA
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri
wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya
vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya
Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana.
Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa
Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na
wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa
Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini
Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria
Februari Mosi, Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akitoka nje ya
ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kutetea na kufafanua vipengele
kadhaa vya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016,
husani eneo la Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana, na baadaye Muswada
huo kupitishwa na Bunge ili uwe Sheria, Februari Mosi, 2017, Bungeni
Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimweleza jambo
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani
(Mb), nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha
Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016,
Februari Mosi, 2017.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkurugenzi wa
Idara ya Sheria wa Wizara hiyo Bi. Suzana Mkapa, Nje ya Ukumbi wa Bunge
Mjini Dodoma, kwa namna alivyoshirikiana na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bw. George Masaju, kufanikisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria
mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge Februari
Mosi, 2017.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akifurahia jambo na
maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara yake baada
ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4
ya Mwaka 2016, uliopitishwa Februari Mosi, 2017, mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha
ya pamoja na Maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara
yake, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya kupitishwa kwa
marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, ikiwemo Sheria
ya Mikopo, Misaada na Dhamana.
Maafisa
Waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wakiambatana na Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Suzana Mkapa
(kulia), wakiwasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kusikiliza
mjadala wa Bunge kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali
Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari
Mosi, 2017.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment