Posts

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi  Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKATWA MAPANGA NA MWALIMU

Image
MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega. “Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo w

MANENO YA ZITTO BAADA YA KUPATA MTOTO WA KIKE

Image
July 14, 2016  Mbunge wa Kigoma mjini,  Zitto Kabwe  aliingia kwenye headlines za kuuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake.  Good news leo December 27 2016 Zitto Kabwe na mkewe wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm Kulthum. Zitto Kabwe amezitoa taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na amesema kuwa wamempa jina hilo kwa heshima ya mwanamama mpigania uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO, aidha amesema Umm Kulthum kwa heshima ya mama yake mdogo na pia jina la binti wa Mtume Muhammad (SAW).

MAGAZETI YA LEOJUMANNE TAREHE 27.12.2017

Image
 

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
 

WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam. Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.  Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.  Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani.  Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani.  Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front  Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na familia yake.  waumi

MAMBO Yanayoshusha Thamani ya Mwanaume Mbele ya Mwanamke

Image
Katika uhusiano baina ya mume na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu. Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele ya mwanamke. Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele ye mwanamke: 1. HADAA NA UNYONYAJI: Baadhi ya wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha mapenzi. Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu matatizo ya kipesa na kiuchumi. Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo. 2. WANAWAKE WENGI: Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume. Kuwa na uhusiano na wanawake wengi

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 25.12.2016

Image