WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM


Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.

Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam.

Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.

 Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.

 Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani.

 Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani.

 Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front

 Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na familia yake.

 waumini wakiwa nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri usharika wa Azania Front baada ya ibada hiyo.

Kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph ikitoa burudani

Na Dotto Mwaibale
AMANI Duniani na hapa nchini hawezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wenye kumcha mungu.
Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akiongoza ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam jana.
"Amani duniani na hapa nchini haiwezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wamchao kristo" alisema Pengo.
Alisema kila mmoja wetu mahali alipo akitekeleza wajibu wake ipasavyo atambue anakuwa anatekeleza amani.
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dk. Alex Malasusa alisema Sikukuu ya Krismasi inamaanisha ni amani na ndio maana watu mbalimbali wamekuwa wakipeana zawadi kuashiria amani hivyo akawaomba wakristo na watu wote kuendeleza amani nchini. 
Katika ibada hiyo ya mkesha wa Krismasi waumini walimiminika kwenye makanisa ya Anglikana la Mtakatifu Albano, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Mtakatifu Joseph na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front huku wakiburudishwa na nyimbo za kusifu mungu za kuzaliwa kristo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)(P.T)

Comments

Popular posts from this blog