Posts

RAIS DKT MAGUFULI ASHUHUDIA RAIS KABILA WA DRC AKIWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE JENGO LA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akihutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wamefanya mazungumzo rasmi Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi mbili marafiki na

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA DHIFA YA TAIFA RAIS JOSEPH KABILA WA DRC, IKULU, DAR ES SALAAM

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwaheshima yake  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwa heshima yake  Rais Joseph Kabila akimwamkia Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake  Rais Joseph Kabila akimwamkia Mama Sitti Mwinyi, Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi,  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt Magufuli kwa heshima yake  Rais Joseph Kabila akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe Anne Makinda