Posts

Yatazame hapa: Majina ya kashfa ya kuficha fedha ughaibuni (Panama Papers) yawekwa wazi.

Image
Kashfa ya kuficha fedha ughaibuni (offshore) maarufu kama Panama Papers imechukua muelekeo mpya baada ya shirika la uandishi wa kiuchunguzi duniani (ICIJ) hii leo kuweka wazi majina na nchi za vigogo wanaohusika na kashfa hii. Kufahamu kuhusu wahusika Tanzania na nchi nyingine bonyeza hapa . Facebook Comments

DKT KIKWETE ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI

Image
Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mw

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITAAGIZA TANI 70,000 ZA SUKARI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Waandishi wa Habari kwenye makazi yake jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano). Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati). “Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au m

EXCLUSIVE: Rachel Kizunguzungu amrudia Mungu… ni baada ya yote aliyofanya na kupitia.

Image
Mwimbaji Rachel ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania ( THT ) na kuanza kuachia nyimbo zake, amekaa kwenye Excluvie na mtangazaji wa Amplifaya ya CloudsFM Millard Ayo na kueleza kilichotokea mpaka akakwama na kukaa kwenye nchi ya watu kwa zaidi ya miezi saba, ishu yake ya kuvuta bangi na mengine. KUHUSU KUMRUDIA MUNGU:   Ni kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva lakini muda mwingi nitautumia kanisani. KUHUSU OMAN: ‘Ni kweli nimekaa nchini Oman kwa zaidi ya miezi saba, nilikwenda kwa ajili ya kufanya shows tu lakini nikapata tatizo kwenye VISA yangu, nilifanya show za kuandaa mwenyewe ikafanikiwa mwanzoni lakini baadae hali ikabadilika, nilikua na VISA ya miezi mitatu na nikae

WEMA SEPETU AFUNGUKA JUU YA MCHEZAJI HARUNA NIYONZIMA

Image
Ibrahim Mussa, Dar es Salaa BAADA ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola, msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amefunguka kuwa hajui ni kwa nini amekuwa akimpenda kiungo wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima. Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Championi Jumatatu lilimshuhudia msanii huyo ambaye pia alikuwa Miss Tanzanani mwaka 2006, akiwa amekaa Jukwaa la VIP A kwa ajili ya kutoa sapoti kwa timu yake hiyo. Akizungumza na Championi Jumatatu, Wema alisema kuwa upendo wake kwa kiungo huyo ni mkubwa mno kiasi kwamba hajui kwa nini inakuwa hivyo, lakini akaongeza kuwa inawezekana kuwa ni kutokana na uwezo wake anaouonyesha uwanjani ambapo katika mchezo huyo aliwapa wakati mgumu viungo wa Esperanca. “Mimi ni shabiki wa Yanga damu kabisa, tangu nazaliwa na utabiri wangu umeenda vizuri, maana nilisema kabla ya mchezo kuwa tutashinda na imekuwa kweli, ushindi huo n

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.  Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia na wanakwaya  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Maguful