Posts

11 Certain Signs He’s Ready For A Serious Relationship.

Image
The beginning of a relationship can be a cloudy thing – it’s hard to determine if someone is just playing you and feeding you words you want to hear, or if they’re sincere and really care about you. Here’s a guide to weeding out the bad guys from the good ones, and seeing who’s willing to go past the casual phase and dive into something real. 1. He’s stopped seeing other people and wants to be exclusive. He wants to see you on Friday and Saturday. He’s so into you, he can’t even think about other girls, because you’re the only one that really makes him happy. He knows building a real foundation with you means getting serious with exclusivity, and he’s into it. 2. He’s starting using the we word. That means he visualizes himself with you, and wants to get serious with you. He wants to make more memories with you, and wouldn’t use that word if he couldn’t see himself with you.  3. He’s open about his insecurities with you. He talks about his struggles, with confide...

Mama Salma Kikwete afunguka maisha yake kama mama

Image
Mke wa rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amevitaja vitu anavyovipenda kufanya akiwa nyumbani. Mama Salma Kikwete ni msimamizi mkuu wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, inayowasaidia kuwasomesha watoto wa kike wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi. Akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa Clouds Media waliomtembelea nyumbani kwake kuelekea siku ya mama duniani, siku ya Jumapili, Mei 8, amesema, “Mimi ni mama wa watoto tisa, kulea watoto tisa haikuwa shughuli ndogo lakini nashukuru Mungu kwa baraka ya kuwapata watoto wangu. Watoto wangu wamekuwa wakisaidiana sana wakati wa kuleana na kushirikiana katika kila jambo. Ukiacha hao tisa nina watoto wengine ninaowasomesha nina watoto wengi sana, nawapenda sana wanangu naamini hata wao wananipenda pia.” Aidha Mama Salma aliongeza, “ninapoona wanangu wanaandikwa vibaya kwenye magazeti, nachukizwa na jambo hilo kama mzazi, lakini natambua haya yanatokana na maisha tuliy...

Walimu wapewa kichapo

Image
Bariadi. Walimu watano wamepigwa na kung’olewa mazao yao mashambani na wanakijiji kwa madai  ya kuwazuia kuchungia mifugo katika maeneo ya shule. Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) wilayani hapa, Baraka Owawa amewaambia waandishi wa habari baada ya kutokea tukio la kati shule za msingi Giriku, Nkindwabiye, Sapiwi na Nyamikoma. Owawa amewataja walimu waliopigwa na wananchi kwa madai ya kuzuia mifungo kufanya malisho katika maeneo ya shule kuwa ni Masumbuko Jackson, George Mwakanusya, Joseph Marco, Zacharia Jeremiah na Hipolitus Domisian ambao walilazimika kukimbia vituo vyao vya kazi. Amesema licha ya kupigwa, walimu hao wamepewa vitisho na wanakijiji wanaojiita wazawa kuwa wanaweza kusingiziwa kuwabaka wanafunzi au kutembea na wake za watu ili kuhalalishiwa tuhuma za kuwapiga.

TAMKO LA WIZARA KULAANI MAUAJI YA MAMA NA MTOTO, B/MOYO

Image
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa, mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi. Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu. Wizara inasisitiza kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa wanafamilia liko mikononi mwa kila mwananchi, hivyo jamii inawajibu wa kusaidia udhibiti wa ukatili na mauaji katika familia na jamii zetu. Jamii ikiwa na uelewa wa pamoja katika haki za wanawake na watoto katika jamii, itawezesha kuwekeza katika haki ya k...

TRA KUGAWA EFD’S 5700 KWA WAFANYABIASHARA

Image
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato nchini kulia ni Kamishna wa kodi za ndani Bw. Yusufu Salum. (Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO) Na Lilian Lundo MAELEZO Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFD’s kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kukusanya mapato nchini. Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo. “ Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na kising...

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI MKOANI MANYARA ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha sehemu mbalimbali wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha kwa njia ya barabara leo Mei 6, 2016. PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magug...

Zifahamu Faida/Hasara za kurudiana na Mpenzi wako wa zamani.

Image
Kuna faida ya wapenzi kuachana na kurudiana? Vipi kuhusu hasara zake? Hiyo ndiyo mada yetu ya leo kama inavyojieleza. Bila shaka unawajua watu ambao walikuwa wakiishi pamoja kimapenzi, iwe ni ndoa, uchumba au uhusiano wa kawaida ambao wamewahi kutengana na baadaye wakarudiana, iwe ni mara moja au zaidi. Yawezekana hata wewe ukawa miongoni mwa watu wa aina hiyo, kwamba uliwahi kutengana na mtu umpendaye lakini baadaye ukajikuta unarudiana naye na kuanzisha upya uhusiano. Je, kuna faida na madhara gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi unawachukuliaje? NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MAPENZI Yawezekana aina hii ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya muda mkarudiana tena, likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi za Kiafrika lakini kwa taarifa yako, hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano w...

JOYCE KIRIA AMLILIA KIKWETE AZUNGUMZA MAZITOO

Image
 Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria. Ameandika kwenye page yake ya Facebook ''Dady i miss u 😭. pesa imestaafu na wewe, maisha magumu kweli, siku hizi pesa naiona kwenye taarifa ya habari, habari za biashara ''

HATIMAYE Snura awaomba radhi Watanzania, awasilisha video safi ya Chura kukaguliwa

Image
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Snura akiongea na waandishi wa habari Alhamis hii Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Jana video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA. Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania ambayo itaikagua.

Kikwete 'Agoma' Kumkabidhi Rais Magufuli Chama......Mwinyi,Mkapa,Malecela Kukutana kwa Dharura Kumjadili

Image
Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu. Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho. Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli. Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hich...

REAL MADRID WAICHAPA MAN CITY KWA BAO 1-0 NA KUTINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Image
Real Madrid imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 jijini Milan, Italia. Madrid imetinga fainali baada ya kuitwanga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid. Bao la Madrid limepatikana baada ya shuti la Gareth Bale aliyekuwa akipiga krosi kumgonga Fernando na kujaa wavuni. Pamoja na Madrid kutinga fainali, maana yake Kocha Zinedine Zidane ameandika rekodi yake ya kwanza kucheza fainali hiyo, safari hii akiwa kocha. Lakini Man City imeishia nusu fainali iliyokuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia Ushindi huo wa bao 1-0, unaipitisha Madrid hadi fainali baada ya sare ya bila bao katika mechi ya kwanza jijini Manchester.

Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

Image
TAARIFA YA MAUAJI.BAG/IR/1078/2016.MNAMO 04/05/2016 MAJIRA YA SAA 16.30HRS HUKO KAOLE KWENYE VICHAKA KATA YA DUNDA (W)B'YO(M)PWANI OLVER S/O ERASTO,22YRS,MCHAGA,MKULIMA, WA KAWE DSM NA MTOTO WAKE EMMANUEL S/O FROWIN PETER,3YRS MHEHE WOTE WALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA KISU NA MME WAKE FROWIN S/O PETER,MBWALE,26YRS,MHEHE,DEREVA,MKAZI WA KAWE DSM AKISHIRIKIANA NA RAFIKI YAKE RAJABU S/O JUMA,20YRS,MKULIMA,MKAZI WA MAKONGO DSM.MIILI YAO IMEKUTWA UMBALI WA MITA 100 KUTOKA BARABARANI.CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA MAPENZI AMBAPO MUME WA MAREHEMU ALIMUHISI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MTU AITWAYE HAMZA S/O ? MKAZI WA KAWE DSM .MBINU ALIMDANGANYA KWAMBA WAODOKE PAMOJA NA MTOTO WAO KWENDA KAOLE BAGAMOYO KUANGALIA NYUMBA YAO ANAYOENDELEA KUJENGA WALIKODI PIKIPIKI MC 235 AWR FECON HADI KAOLE PORINI.WATUHUMIWA WAMEKAMTWA NA WAMEKIRI KUFANYA MAUAJI HAYO = Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa ki...

BREAKING NEWS : SNURA AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SANAA,VIDEO YA CHURA YATAKIWA KUFUTWA MTANDAONI

Image
 snura katika pozi Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiongea na waandishi wa habari Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar. Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.

Sumaye Amkejeli Rais Magufuli kwa kazi anayofanya

Image
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.   “Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.   “Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiw...

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma...