TRA KUGAWA EFD’S 5700 KWA WAFANYABIASHARA
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akizungumza na
waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya
mapato nchini kulia ni Kamishna wa kodi za ndani Bw. Yusufu Salum.
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
Na Lilian Lundo MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices)
EFD’s kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za
Serikali katika kukusanya mapato nchini.
Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.
Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.
“
Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo
imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa
risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na
kisingizio cha kutokuwa na mashine hizo”. Alisema Kidata.
Kamishna
Kidata ameongeza kuwa Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo na zipo
tayari kuanza kugawiwa mwezi huu kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni awamu
ya kwanza ya ugawagaji wa mashine hizo ambao utafanyika nchi nzima.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za kuweza
kukusanya mapato yatokanayo na kodi za biashara kwa urahisi na ufanisi
mkubwa.
Comments
Post a Comment