Wabunge MABUBU Kubanwa Bungeni......Ni Wale Wanaoshiriki Vikao vya Bunge Lakini Hawachangii Chochote
Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee. Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho. Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11. Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho. Hi