Posts

Fahamu mbinu 10 za vigogo kusafirisha unga

Image
Viatu vya kimasai  na zana nyingine zinazotumika kama urembo ambavyo vimetajwa kama zana muhimu zinazotumiwa katika usafirishwaji wa madawa hayo. Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Tanzania kwenye viwanja vya ndege vilivyopo nchini limekuwa likipambana na wauza madawa ya kulevya ‘unga’ kwa kugundua na kuzima mbinu zote wanazotumia kusafirisha biashara hiyo haramu, hivyo kupunguza kasi ya uingizwaji na utoaji wa unga kwa njia ya ndege, UWAZI limeambiwa. Akizungumza na gazeti hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika wiki iliyopita Makao Makuu ya Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania yaliyopo jijini Dar, Kamanda wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno  (pichani) alizitaja mbinu kumi wanazotumia wauza unga hao kusafirishia bidhaa hiyo. “Kwanza napenda kuweka wazi kuwa, kwa sasa hatuna mchezo na wauza unga. Mbinu zao zote wanazotumia kusafirishia madawa yao tunazijua. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambi...

CLOUDS FM YAIBOMOA RADIO YA MENGI EA RADIO KWA KUMCHUKUA DJ MAARUFU NA MTANGAZAJI WA RADIO HIYO

Image
Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya. DJ Sinyorita na Mami Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM. Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida. Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo. Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio. Wawili hao wanatarajiwa kutambulishwa rasmi kwenye kituo chao kipya cha kazi soon.

Kigwangalla atembelea hospitali ya Haydom Mbulu-Manyara

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Khamisi Andrea Kigwangalla akielezea machache juu ya ujio wake katika hospitali hiyo.  Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kitengo cha Macho katika Hospitali hiyo ya Hydom. …Akipata maelezo juu ya kitengo maalum cha ufundi wa vifaa tiba. …Akipata picha ya pamoja na mtaalam wa masuala ya ufundi wa vifaa tiba vya kitaalam. …Akiangalia chumba cha CT-SCAN. Mashine ya kisasa ya CT-SCAN iliyopo katika hospitali hiyo ya Hydom.  …Akitembezwa katika moja ya wodi za hospitali hiyo. …Akiwasili katika Chuo cha Uuguzi cha Hydom kinachomilikiwa na Hospitali hiyo ya ya Hydom. …Akiwa katika Chuo cha Uuguzi. …Akisikiliza kwa risala fupi kutoka kwa msimamizi wa chuo hicho. …Akitoa maelezo kadhaa kwa uongozi wa Hospitaali hiyo baada ya kumaliza kuitembelea. Wanafunzi  wakifuatilia mkutano huo. Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo akiuliza sw...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 12.04.2016

Image

RAIS DK. MAGUFULI AAGIZA BILIONI 6 KUTOKA BUNGE ZIKABIDHIWE KWA MAGEREZA NA JKT ILI KUTENGENEZA MADAWATI 120.000

Image
Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo. Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati. Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka. Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapi...

Bulembo: Lowassa ni Fisadi, Namshauri Amwache Rais Magufuli na Badala yake Aende Kijijini Kuchunga Ng'ombe

Image
Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo amemtaka waziri mkuu wa zamani Edward  Lowassa  amwache Rais Magufuli aendelee kufanya kazi zake. Bulembo anakuwa kiongozi wa pili wa CCM kumvaa Lowassa aliyekosoa utendaji wa Rais  Magufuli  wa kutumbua majipu wakati  alipokutana na wanazuoni wa ndani na nje ya nje Alhamisi ya wiki hii, baada ya juzi  msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka  naye kumkosoa kuwa si kweli  kwamba watumishi wa umma wanafukuzwa bila kusikilizwa. Akizungumza  mjini  hapa jana na wanachama wenzake wakati wa maadhimisho ya miaka 61  ya Jumuiya  hiyo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro, Bulembo  alimtaka Lowassa  kutekeleza ahadi yake ya kwenda  Monduli kuchunga  ng'ombe  kama hatochaguliwa kuwa Rais. "Kama yeye anasema kasi ya Magufuli ni ya muda au anakosea kutumbua majipu, basi tunamkumbusha kauli yake wakati akiongea na...