Posts

BOSI WA ZAMANI WA TRA HARRY KITILLYA, SHOSE SINARE NA SIOI SOLOMONI WANYIMWA DHAMANA

Image
Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande. Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic. Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao. Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu. Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosa

Ujumbe mzito wakutwa kaburini kwa Kanumba!

Image
Ujumbe uliokutwa kaburini kwa Kanumba. Stori:  Mayasa Mariwata na Gladness mallya, Ijumaa Wakati mama yake, Flora Mtegoa (pichani), baadhi ya wasanii na mashabiki wake wakikumbuka miaka minne ya kifo cha aliyekuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, kumezuka sintofahamu ya kukutwa ujumbe mzito wa kimapenzi kaburini kwa msanii huyo ambao unadaiwa kuwekwa na mrembo aliyefika mahali hapo mapema wiki hii. TUJIUNGE MAKABURI YA KINONDONI Kwa mujibu wa mtu aliyedai ni mmoja wa walinzi wa Makaburi ya Kinondoni, Dar, alikolazwa Kanumba kwenye nyumba yake ya milele, ishu hiyo ilijiri Jumanne wiki hii, majira ya jioni ambapo mwanadada huyo alionekana akishuka kwenye gari (halikutajwa ni aina gani) na kuelekea kaburini hapo. Mrembo aliyekutwa kaburini. Alisema kuwa, huku akiwa amejitanda mtandio na maua mkononi, baada ya kufika kaburini hapo alionekana akiangua kilio na kuangusha maombi mazito kabla ya kuacha ujumbe na kuondoka zake.

HATIMAYE CCM WAMJIBU LOWASA BAADA YA KUMPONDA RAIS MAGUFULI KWA UTENDAJI WAKE

Image
Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi. Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini. Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla. Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji. Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unaji

BREAKING NEWZZZ.....HATIMAYE EDWARD LOWASSA AANDIKA MANENO HAYA USIKU HUU KUHUSU UTAWALA WA RAIS MAGUFULI

Image
  Hali ya siasa nchini ni ya hamasa, lakini isiyokuwa na misingi endelevu. Kwakuwa Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni bunge. Pia nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwasababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo. Bandari sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga s hughuli zake na pale palikua na vijana wetu wengi wameajiriwa,sasa hivi wako mtaani hakuna mbadala wa ajira, hii inasababisha hali ya maisha ya wananchi yanakua magumu. Kuhusu swala la MCC ni pigo kwa mustakabali wa uchumi, kutaka nchi ya viwanda kunahitaji uwekezaji mkubwa,katika hili fedha tutatoa wapi kama sio wafadhili wa ndani na nje kufanikisha? Hawa wafadhili sio watu wa kuwabeza kwakuwa tunafanya nao miradi mingi ya kimaendeleo na wanavyotoka hivi itaturudisha nyuma, Tunahitaji kujitegemea, ndiyo, ila kwa mipango huku tunatafuta mbadala wa kila msaada. Hapa kinacho

PROFESA MUHONGO ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA NISHATI NA MADINI.

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara yake katika  ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mwenyekiti wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa Solidarity leo katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo wakati wa ufungunzi wa Baraza la wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. WAZIRI wa Nishati

NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) ANG’OLEWA KWA TUHUMA YA KUMILIKI NYUMBA 40

Image
Mkuu  wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu   Mkuu  wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu, amemwondoa kwenye nafasi yake, Mnunuzi wa Vifaa na Boharia Mkuu wa jeshi hilo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Adriano Magayane ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. Kuondolewa kwa DCP Magayane katika nafasi hiyo kunatokana na taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari hivi karibuni, kuwa anamiliki nyumba zaidi ya 40 na kumbi kadhaa za starehe ndani na nje ya Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Gazeti la Mtanzania,  IGP Mangu amefikia uamuzi huo kwa kile kinachodaiwa kuwa tuhuma hizo ni nzito na zinalenga si kumfedhehesha yeye kama ofisa mkuu wa Jeshi la Polisi, lakini kwa jeshi zima. “IGP Mangu amemwondoa mara moja DCP Magayane kutokana na tuhuma zinazomkabili, kwa kweli ni nzito, nadhani hatua zilizochukuliwa ni sahihi… unajua sisi askari tuna miiko ya utendaji kazi, sasa inapotokea tuhuma kama hizi kwa ofisa kama huyu, lazima uchunguzi wa ki

TAZAMA PICHA ZA MELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI

Image
Longer than The Shard and wider than a Boeing 747 wingspan: The world's largest cruise ship arrived in the UK today for the first time.

BINTI MWENYE ULEMAVU AFUNGIWA NDANI MIAKA 16

Image
Vitendo vya kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu limeendelea kushamiri kwenye maeneo mengi nchini tukio la sasa likitokea katika kijiji cha njani wilayani Arumeru ambapo mtoto wa kike mweye ulemavu wa viungo amebainika kufungiwa ndani kwa kipindi cha umri wake wote wa miaka kumi na sita. Mtoto huyo Wine Ruth anayelelewa na bibi yake baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi mara baada tu ya kugundua kuwa ana ulemavu amegundulika wakati wa zoezi la kuwaorodhesha watoto wenye ulemavu wilayani Arumeru ambapo bibi yake Veraelly Ndetaulo anakiri kumfungia kwa ajili ya usalama wake anapokwenda kuwatafutia rizi wajukuu zake. Akizungumzia tukio hilo Mbunge wa Viti Maalum Walemavu Dk.Elly Macha aliyeongoza zoezi la kumtoa ndani mtoto huyo anasema imefika wakati sasa jamii ikatambua kuwa malezi ya watoto wa kundi hilo ni la kushirikishana hasa ikizingatiwa kuwa wengi wamekua wakitokea kwenye familia zenye kipato duni. Maisha ya Bibi Ndetaulo anayemlea mtoto huyo mwenye ulemavu,pa

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUMBUKUMBU YA KARUME ZANZIBAR

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi wa ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo    inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo    inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, ambapo  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli ambaye yuko nje ya nchi kikazi.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kulia na Viongozi mbalimbali