SAKATA la Mabosi wa NHC na EWURA Kulipwa Mshahara wa Milioni 36 Lachukua Sura Mpya Baada ya Wenyewe Kukana
Mabosi wa mashirika mawili ya Serikali nchini, wanaodaiwa kulipwa mshahara wa Sh milioni 36, wamekanusha madai hayo, huku wakielezea kushangazwa na taarifa hizo wakati hata nusu ya fedha hizo, hawapati. Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu alisema halipwi mshahara huo. Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu taarifa ya utekelezaji na utendaji wa shirika hilo kwa mwaka 2014/15, Mchechu alisema shirika hilo pamoja na kutekeleza majukumu yake, bado lina changamoto za uhaba wa fedha. “Katika ujenzi wa nyumba zetu, Serikali haigharamii masuala ya miundombinu kama vile maji, umeme, barabara hilo ni jukumu letu na linatugharimu fedha nyingi. “Sasa nashangaa wako watu wanasema mimi nalipwa mshahara mkubwa, sielewi wametoa wapi huo mshahara kwa sababu silipwi mshahara huo, mimi nali