Posts

UKAWA WASHINDA KITI CHA UMEYA MANISPAA YA ILALA.

Image
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam. Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya  wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi  wa kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya,naibu Maya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Ume

HATUA AMBAZO ZIMECHUKULIWA DHIDI YA STANBIC BANK TANZANIA LIMITED KUHUSU USHIRIKI WAKE KUWEZESHA MKOPO WA SERIKALI WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 600

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani)jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Benki ya Stanbic Tanzania kutokana na ushiriki wake katika kuwezesha mkopo wa Serikali wa Dola za Kimarekani Milioni 600 na Kulia kwake ni Naibu Gavana  wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Bw. Lila Mkila. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (katikati)  akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kusudio la kuitoza Benki ya Stanbic faini ya shilingi bilioni 3.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile na Kushoto kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lila Mkila. ……………………………………………………………………………………… Utangulizi Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusiana na hasara i

Vidokezo · Tanzania

Vidokezo · Tanzania

AUNT EZEKEL MKE WA IYOBO WAPATANA

Image
 Mwigizaji Aunt Ezekiel akiwa na mke wa Iyobo. DAR ES SALAAM: Yamekwisha! Baada ya kudumu ndani ya bifu kwa muda mrefu huku wakituhumiana uchawi, hatimaye mwigizaji Aunt Ezekiel na mzazi mwenzie na Moses Iyobo, Mwengi Ally wamekutana na kumaliza tofauti zao. Mapema mwaka jana, wawili hao waligombana kufuatia Iyobo ambaye ni dansa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kummwaga Mwengi kisha kuanzisha uhusiano na Aunt ambapo uhusiano huo ulijibu na wakafanikiwa kupata mtoto. Aunt ndiye aliyeamua kufuta ‘kinyongo chao’ ambapo alisema hakuona sababu ya wao kuendeleza bifu lisilokuwa na msingi wowote na kuwa wao ni wazazi na watoto wao ni ndugu wa damu moja, alimshauri Iyobo awakutanishe, wamalize tofauti zao.   Baada ya kukubaliana, Aunt na Mwengi walikutana katika Hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar wakiwa na Iyobo ambaye alisimamia zoezi zima la mapatano kwa wawili hao kuzungumza, wakaelewana, ‘wakazika’ tofauti zao n

RAIS MAGUFULI AENDELEA KUTUMBUA MAJIPU,KIGOGO MWINGINE ATUNBULIWA JIJINI MWANZA

Image

KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHIRISHWA

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi. Na:George Binagi-GB Pazzo Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu.  Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 16.01.2016

Image
  MAGAZETI YA UDAKU LEO   MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI v

KAJALA ADAIWA KUNASA UJAUZITO WA KIGOGO MKUBWA,MENGI YAFICHUKA

Image
Mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’. Mwandishi Wetu, Huenda mambo yanaweza yakawa yamejipa kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ kwani kuna taarifa zinadai kuwa mwigizaji huyo amenasa mimba ya kigogo serikalini. Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo ambaye ana mtoto mmoja aliyezaa na prodyuza mkongwe Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’ (Paula), kimepenyeza ubuyu huo kuwa Kajala ana mimba ya zaidi ya miezi mitano na amegusiwa kuwa ni ya kigogo serikalini ambaye hataki kumtaja jina. “Hivi hamna habari? Kajala mbona mjamzito. Tena yeye alianza kunasa kabla hata ya Wema, nashangaa mnakomalia kuripoti mimba ya Wema tu, Kay mmemuacha na kigogo wake,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho. Baada ya kupewa ubuyu huo, juzi Alhamisi, mwanahabari wetu wakati anaanza kuichimba habari hiyo, alitembelea kwenye ukurasa wa Instangram wa Kajala na kukutana na ujumbe ulionesha dhahiri kuwa mwigizaji huyo anajiandaa kuitwa mama kwa mara nyingine. “Hey IG...do me a favor...help me to choose

MILIPUKO YA MABOMU YAUWA WATU ZAIDI YA 7A INDONESIA

Image
Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo. Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa. Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano. Polisi wa Indonesia wakijihami Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN). Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara. Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama. Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”. “Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa hiki,