Posts

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukum

BREAKING NEWZZZZ!! KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA LEO,JAMES LEMBELI APENYA KIZINGITI CHA KWANZA

Image
Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka 2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Tanzania Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli

WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.

Image
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu. Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi w

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 08.12.2015

Image
       N,

MUHUMBILI YAPATIWA MSAADA WA MASHINE YA KISASA YA DIGITAL YA X-RAY

Image
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia. Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika. Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). ……………………………………………………………………………… Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutu

NEC YATAOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA WABUNGE ARUSHA MJINI NA HANDENI

Image
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

MAGUFULI ATAJWA HUKO SWEDEN KUWACHONGANISHA MARAIS WENZAKE NA WAPIGA KURA WAO

Image
Dagens Nyheter ni gazeti kubwa kushinda yote nchini Sweden, ndio 'Daily News' lao kwa maana ya jina la gazeti. Katika toleo lake la Ijumaa Desemba 4, habari za John Magufuli zimepamba pia gazeti hilo. Amemwagiwa sifa, na ikaandikwa pia, kuwa Magufuli amewaweka katika wakati mgumu marais wenzake wa nchi jirani kwa vile wapiga kura wao wameonyesha wivu wao kwa Watanzania kupata Rais wa aina ya Magufuli. Hata hivyo, kwenye gazeti hilo, imeandikwa pia, kuwa hata kabla ya kuingia milango ya Ikulu, Magufuli tayari ameshajipatia maadui wakiwamo wa ndani ya chama chake kwa hatua zake anazozichukua, hususan za kubana matumizi ya Serikali.  Habari nzima  unaweza kuitazama kupitia Website ya Hilo gazeti kwa kubofya link hii hapa .Imeandikwa kwa lugha yao. link: http://www.dn.se/nyheter/varlden/president-skaffar-fiender-nar-han-later-kvasten-ga/ Tafsiri ya maelezo waliyoandika  kwa Kiingereza ni kama inavyosomeka hapa chini...... The newly elected Presiden

SAKATA LA MANJI NA COCO BEACH, TAMKO KALI LATOLEWA,WAFUNGUKA MAZITO,HATUA KALI KUCHUKULIWA

Image
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ndugu waandishi wa habari, Jukwaa limewaalika hapa katika muendelezo wake wa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. -Dr. John Magufuli. Hivi karibuni mh. Rais ameongoza mapambano makubwa ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi yaliyopotea. Tunaunga mkono juhudi hizi za Rais wetu na tunamuhakikishia kuwa Jukwaa linamuunga mkono na kwamba tunaomba azidishe kasi zaidi ili wale wote waliokwepa kodi wakamatwe, walipe na kufikishwa katika vyombo vya sheria bila huruma yoyote. Ndugu waandishi wa habari, leo tumewaita hapa dhumuni kuu likiwa ni kuzungumzia uporaji wa maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi hasa wanyonge. Uporaji huu unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa ambao hutumia nguvu zao za kiuchumi kuwarubuni na wakati mwingine kuwahonga viongozi wetu wachache seri

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) LEO

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe. Kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika. Akizungumza  na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa ut

KATIBU MKUU TAMISEMI AKAGUA MIUNDOMBINU YA MFUMO WA MABASI YAENDAYO HARAKA

Image
  Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwisho mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi 140. Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akikagua miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendeyo haraka na kuli ni Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwishoni mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi

KORTINI KWA TUHUMA NJAMA ZA KUTAKA KUMUUWA MWENYEKITI WA NEC JAJI LUBUVA

Image
WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake. Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba. Wakili wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia yake. Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashi

BREAKING NEWZZZ!!!! ABOUBAKAR KASONGO MPINDA ‘CLAYTON’ AFARIKI DUNIA

Image
King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake. Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia). Na Sifael Paul Habari zilizoufikia mtandao huu jioni hii zinaeleza kuwa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar. Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo ambaye alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na Nyimbo za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake. Katika siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala Asssosa.

BREAKING NEWS : KESI ILIYOKUWA INAMKABILI MWENYEKITI WA CUF IBRAHIM LIPUMBA YAFUTWA RASMI

Image
Professor  Ibrahim Lipumba  alikuwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi. Picha ya January 2015  Prof. Lipumba  akiwa Mahakamani Kesi hiyo ilianza kusikilizwa toka January 2015, ninayo ripoti kutoka kwenye taarifa ya habari ya ITV kwamba  Prof. Lipumba  na watu wote 30 wamefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili Mahakamani hapo.