ACHENI RUSHWA TUISAIDIE NCHI IPATE MAENDELEO, MAGUFULI.
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara Ujenzi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo. Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza leo jijini Dar es Salaam,katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya ujenzi. Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi waliohudhuria katika ufunguzi wa baraza hizo leo jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja ya waziri wa Ujenzi pamoja na Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi. Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii WAZIRI wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli amewataka wafanyakazi katika wizara hiyo kuacha rushwa na badala yake wafanye kazi kwa weledi katika kusaidia nchi kuendelea katika ujenzi wa barabara. Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo,amesema wizara hiyo imekuwa na mafanikio kutukana na wafanyakazi kujituma katika miradi mbalimbali