ACHENI RUSHWA TUISAIDIE NCHI IPATE MAENDELEO, MAGUFULI.
Waziri wa
Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la
wafanyakazi wa wizara Ujenzi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es
Salaam leo.
Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza leo jijini Dar es Salaam,katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya ujenzi.
Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi waliohudhuria katika ufunguzi wa baraza hizo leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya
pamoja ya waziri wa Ujenzi pamoja na Baraza la wafanyakazi wa wizara ya
ujenzi. Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Na
Chalila Kibuda,Globu ya Jamii WAZIRI wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli
amewataka wafanyakazi katika wizara hiyo kuacha rushwa na badala yake
wafanye kazi kwa weledi katika kusaidia nchi kuendelea katika ujenzi wa
barabara.
Magufuli ameyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Baraza la wafanyakazi wa
wizara hiyo,amesema wizara hiyo imekuwa na mafanikio kutukana na
wafanyakazi kujituma katika miradi mbalimbali.
Amesema madaraja
na barabara yaliyokuwa yakisumbua tangu nchi ipate uhuru yamekamilika
katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Jakaya Kikwete na miradi mingine
inaendelea ambayo Tanzania itakuwa nchi ya kuigwa katika kwa kuwa
madaraja ya juu.
Aidha
amesema Wizara ya ujenzi imevuka hata ilani ya uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) kutokana na kutekeleza miradi kwa asilimia 91.
Magufuli
amesema katika sekta ya usafirisha kwa njia ya barabara ndio inabeba
uchumi kutokana na kutegemea kwa asilimia 99.7 huku usafiri wa Reli,Maji
na Anga ikiwa na asiliamia 0.7.
Magufuli
amewataka wafanyakazi kuacha kulalamika kwani wanaweza kulalamika hata
kama vitu vinavyofanywa ni vizuri na hiyo ndio umekuwa utamaduni wa
watanzania.
Amesema
kwa vivuko vilikuwa 15 lakini sasa viko 30 hali ambayo imerahisisha
usafiri kwa wakazi wanaotumia vivuko na kufanya maeneo hayo kukua
kiuchumi.
Comments
Post a Comment