NGUMI ZAPIGWA BUNGENI NCHINI KENYA
Seneta Johnston Muthama aliyejeruhiwa mguuni na kuchaniwa suruali yake wakati wa vurugu bungeni leo. WABUNGE nchini Kenya leo wametofautiana bungeni na kuamua kutupiana makonde huku wengine wakichaniana nguo kufuatia mjadala kuhusu muswada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa Wakenya. Bunge nchini Kenya. Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 kufuatia mtafaruku huo. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha muswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais Kenyatta kuwa sheria. Wabunge wa upinzani waliupinga muswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kutaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa muswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa muswada huo wakisema 'bado mapambano.' Spika wa Bunge hilo, Justin Muturi kuna kipindi alimuru wali