TALIBAN WAUA WATU 126 WAKIWEMO WANAFUNZI ZAIDI YA 100 NCHINI PAKISTANI


Majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma za kitabibu.
Mmoja wa wanafunzi aliyejeruhiwa na Taliban akipatiwa huduma ya kwanza.
Majeruhi akipatiwa huduma katika hospitali jijini Peshawar nchini Pakistani.
Ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika mitaa ya Jiji la Peshawar.
Magari ya kubeba wagonjwa wakielekea eneo la tukio.
Wananchi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa mwanafunzi mmoja aliyeuawa na Taliban.
Wanajeshi wakiwasili eneo la tukio.
TAKRIBANI watu 126 wameuawa, wakiwemo wanafunzi zaidi ya 100, baada ya wapiganaji sita wa Kundi la Taliban waliokuwa wamejihami kwa silaha kuvamia shule moja inayomilikiwa na jeshi jijini Peshawar nchini Pakistani na kupiga risasi hovyo na kujilipua kwa mabomu.Shambulio hilo lilianza kwa wapganaji hao kuingia katika shule yenye wanafunzi 500 ambao ni wa grade 1-10 wanaodhaniwa kuwa na umri kati ya miaka 5-14 mapema leo na kuanza kuwapiga risasi hovyo kwa kuingia darasa moja baada la lingine.
Makomando wa Kijeshi walionekana wakifika eneo hilo na kuanza kutupiana risasi na wapiganaji hao.
Baadhi ya wanafunzi bado wanashikiliwa mateka na wapiganaji hao na mapigano hayo yameendelea kwa takribani saa 3 baada ya uvamizi huo.
Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa wapiganaji watatu bado wapo eneo la tukio huku watatu kati yao wakidaiwa kuuawa na makomando.
Waziri Mkuu wa Pakistani, Nawaz Sharif, ameyaita mauaji hayo kuwa janga la kitaifa na yupo njiani kuelekea eneo la tukio.

Taliban wamethibitisha kuhusika na shambulio hilo.

Comments

Popular posts from this blog