Posts

UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU.

Image
 Kijana Lawrent Lawrian, akiwa na uvimbe wa ajabu kichwani mwake. Lawrent Lawrian, 42 (pichani), ni mkazi wa Kijiji cha Nyakisogo, Wilaya ya Biharamlo, mkoani Kagera, amekuwa mwenye huzuni na kukosa raha kwa muda wa miaka 35 kutokana na gonjwa la ajabu linalomtesa ambalo limemsababishia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutoendelea na masomo.  Gonjwa hilo la ajabu ni uvimbe kama nundu kichwani wenye uzito wa kilo 3, ulimuanza akiwa darasa la kwanza.Akielezea zaidi kwa njia ya simu hivi karibuni Lawrent alisema:  “Gonjwa hili lilianza kama kauvimbe nikiwa na umri wa miaka saba, wakati huo nilikuwa na wazazi wote na ilipofika mwaka 1992 baba akafariki dunia.  “Nikabakia na mama tukawa tunaishi kwa kutegemea kilimo cha kawaida, nilikuwa nikienda shule lakini ilifikia hatua nilishindwa kutokana na maumivu na manyanyaso.  “Darasa la saba nilimaliza kwa tabu sana, kwani wanafunzi wenzangu walikuwa wakinicheka na kunitenga, licha ya kuadhibiwa na walimu lakini hawakuacha t

MJOMBA AIBA MKE WA MPWA WAKE ,WAPIGANA,MCHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU,

Image
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake. TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani. Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.  Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.  MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema: Kelvin (kulia)'akidili'  kisawasawa  na mjomba wake.  “Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.” Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin

ANGALIA PICHA DIAMOND, LADY JAY DEE WANGARA TUZO ZA AFRIMMA

Image
Diamond akiwa na tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki. Diamond akiwa na Davido. STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki ndani na nje ya nchi baada ya kutwaa tuzo ya AFRIMMA 2014 ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki. Diamond wakati akielekea kwenye ukumbi  linapofanyika zoezi la utoaji tuzo za Afrimma. Tuzo hizo za Africa Music Magazine (AFRIMMA) zimetolewa leo alfajiri jijini Texas nchini Marekani. Staa huyo alikuwa anawania tuzo katika vipengele vitano ambavyo ni: Msanii bora wa mwaka Afrika, Wimbo wa mwaka, Collabo bora, Video bora ya mwaka na Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki. WASHINDI WA TUZO HIZO ZA AFRIMMA 2014 NI KAMA IFUATAVYO: Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana) Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya) Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria) Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania) Best Male W

CHANZO DIDA KUACHANA NA MUMEWE SASA SIO SIRI TENA

Image
Dida na Ezden wakifunga ndoa July,2013 Dida Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani amefunguka Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm  inayoongozwa na Fadhili Haule na kueleza chanzo cha ndoa yake  na Ezden ‘The Rocker’ Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu. Dida ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi mkubwa kati yao ni simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka kuitumia kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao.  “Tatizo kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa lilikuwa ni simu. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa tuko kawaida, unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo mimi nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha kawaida. Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize. nikamuita, tulikuwa tunaitana ‘ mshik

Bilal awaongoza maelfu ya Waumini wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar leo

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.CHANZO MTAA KWA MTAA BLOG Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.  Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mn

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 24.07.2014

Image