MJOMBA AIBA MKE WA MPWA WAKE ,WAPIGANA,MCHEPUKO SIO DILI BAKI NJIA KUU,
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:
“Mimi
ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake
wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo
hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin asizidi kumjeruhi mjomba wake.
OFM KAZINI, AIBU!
Kufuatia
taarifa hiyo, mkuu wa zamu wa OFM aliwaagiza mapaparazi wake wanaotumia
pikipiki ziendazo kasi ambao walitumia muda usiozidi robo saa kutoka
walipokuwa kufika eneo la tukio ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba
‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana
huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo
lililomtia aibu!
Mjomba akiwa chumba cha gesti mara baada ya mkong'oto 'hevi' kutoka kwa mpwa wake.
PICHA ZA TUKIO
Mapaparazi
wetu bila kuzubaa nao walianza kuchukua picha za tukio hatua kwa
hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe
kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi
asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
MKE ATIMKA KINYEMELA
Katika hali ya kushangza, wakati
wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na
kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.
...Mjomba taratiiibu 'akirejesha' mavazi mwilini mwake.
MLINZI WA GESTI
Timbwili
la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina
halikujulikana) ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na
kuwaweka kitako.
MJOMBA MTU AGOMA KWENDA POLISI
Baada
ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu
alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi
kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa
makusudi.
CHONDECHONDE KELVIN
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia
tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia
kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na
kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe. MJOMBA ‘AJIKOMITI’ KIMAANDISHI
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa
gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye
‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi
laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Sehemu ya nyaraka ikionyesha mjomba 'akijikomiti' kimaandishi.
Katika
barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa
Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha
kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.
MGONI AGEUKA NA KWENDA KUFUNGUA KESI
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati
tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi
(jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe
Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa sababu kisa hiki kinadaiwa kufikishwa
polisi na Joseph, magazeti pendwa ya Global yataendelea kukifuatilia ili
kujua mwisho wake. Endelea kusoma.
Comments
Post a Comment