Posts

ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAPA

Image
                       BOFYA HAPA KUONA MATOKEO HAYO

WAZIRI MAKALLA ATOLEWA CHINI YA ULINZI WA POLISI BAADA YA MKUTANO WAKE KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA

Image
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG  Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.  Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya

MAHAKAMA YAMSAKA PADRI ANAYEKABILIWA NA KESI YA KUMLAWITI MTOTO

Image
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, limeshindwa kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Padri wa Kanisa Katoliki, Sixtus Kimaro aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 17. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa hivi karibuni lakini hata hivyo padri huyo pamoja na wakili wake hawakufika mahakamani. Upande wa Jamhuri una hoja saba katika rufani hiyo.Kabla ya kuachiwa huru baada ya kukata rufaa, Padri Kimaro alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela na kulipa faini ya Sh milioni mbili kwa mtoto baada ya kupatikana na hatia. Kutokana na kushindwa kwa jopo hilo kusikiliza rufani hiyo wiki iliyopita, kwa kutotokea mahakamani hapo padri huyo wala wakili wake, jopo limeagiza upande wa Jamhuri kutoa taarifa ya mwito kuwa anahitajika mahakamani hapo kupitia vyombo vya habari.   Hatua ya kuamriwa kutumika vyombo vya habari kunatokana na wakili wa Serikali, Salum Malick kudai kuwa amepata