MAHAKAMA YAMSAKA PADRI ANAYEKABILIWA NA KESI YA KUMLAWITI MTOTO
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya
Rufaa, limeshindwa kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri
kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Padri wa Kanisa
Katoliki, Sixtus Kimaro aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto
wa miaka 17.
Rufaa hiyo
ilipangwa kusikilizwa hivi karibuni lakini hata hivyo padri huyo pamoja
na wakili wake hawakufika mahakamani. Upande wa Jamhuri una hoja saba
katika rufani hiyo.Kabla ya kuachiwa huru baada ya kukata rufaa, Padri
Kimaro alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela na kulipa faini ya Sh
milioni mbili kwa mtoto baada ya kupatikana na hatia.
Kutokana na kushindwa kwa jopo hilo kusikiliza rufani hiyo wiki
iliyopita, kwa kutotokea mahakamani hapo padri huyo wala wakili wake,
jopo limeagiza upande wa Jamhuri kutoa taarifa ya mwito kuwa anahitajika
mahakamani hapo kupitia vyombo vya habari.
Hatua ya
kuamriwa kutumika vyombo vya habari kunatokana na wakili wa Serikali,
Salum Malick kudai kuwa amepata taarifa kutoka kwa msajili wa mahakama
hiyo kuwa, hati ya mwito wa kumtaka afike mahakamani hapo ilipelekwa kwa
Kanisa Katoliki.
Alidai
kwa mujibu wa taarifa hiyo ya msajili wa mahakama, hati hiyo ilipelekwa
Jimbo Kuu la Dar es Salaam lakini waliambiwa na jimbo hilo kuwa Padri
Kimaro si mwajiriwa wao na wala hawajui alipo.
Jopo la
majaji hao watatu ambao ni Engela Kileo, Steven Bwana na Sauda Mjasiri,
limeamrisha mwito huo umtake afike kusikiliza rufaa yake kwa tarehe
nyingine itakayopangwa na mahakama hiyo.
Akitoa
amri hiyo, Jaji Kileo alisema endapo padri huyo hatafika mahakamani
baada ya matangazo hayo, rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa upande mmoja.
Katika
kesi ya msingi, Padri Kimaro alikuwa anakabiliwa na mashitaka matatu;
kumlawiti mtoto wa miaka 17, shambulio la aibu na kumdhalilisha mtoto
huyo.
Ilidaiwa
kuwa usiku wa Mei 18 mwaka 2005 katika eneo la Changanyikeni, Dampo,
Padri Kimaro alikamatwa na askari aliyekuwa doria, akitenda makosa hayo.
Katika
hukumu iliyotolewa Agosti 9, 2006 na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa
mahakama hiyo, Pelagia Khaday, Padri Kimaro alipatikana na hatia
katika makosa yote na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela na
kulipa fidia ya Sh milioni mbili kwa mtoto aliyeathirika na kitendo
hicho.
Alikata
rufaa Mahakama Kuu iliyosikilizwa na Jaji Robert Makaramba, ambapo
aliachiwa huru baada ya Jaji huyo kudai kuwa hakukuwa na ushahidi wa
kutosha kumtia hatiani.
Hata
hivyo upande wa Jamhuri umekata rufaa kupinga uamuzi huo wa kuachiwa
huru kwa padri huyo wakiwa na hoja saba ya msingi, ikiwa ni kwamba Jaji
aliyesikiliza rufaa hiyo alikosea kisheria na kiusahihi kueleza kuwa
hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuhusu walichokuwa wakifanya mjibu
rufani (padre) na mtoto huyo eneo la Dampo.
Comments
Post a Comment