Posts

ANGALIA PICHA ZA RAY C AKIWA MTAANI LEO, KUHAMASISHA MATEJA KUACHA UNGA

Image
  Leo Ray C Foundation tuliwatembelea waathirika wa madawa ya kulevya Kinondoni!!! nimeongea nao sana na kuwahamasisha waje kupata Tiba ya Methadone Mwananyamala.... nimefurahisana kuskia kutoka Kwao kwamba na wao wamechoka na Maisha ya utumwa...... Tuko pamoja nao kuhakikisha tunawasaidia....... Ray C Foundation Pamoja inawezekana...  

MAJIBU YA ZITTO BAADA YA KUHUSISHWA KUWANYONYA WASANII WA KIGOMA ALL STARS.

Image
Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.  Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF.  Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.  Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi zao mbalimbali.  Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande

WATUHUMIWA WA MLIPUKO WA MABOMU JIJINI ARUSHA WAPANDISHWA KIZIMBANI

Image
Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao. Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi. WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi. Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. CHANZO MTAA KWA MTAA Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni 12 Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruh

HIZI NDIO PICHA NA LIST YA WASANII WA BONGO MOVIE WALIOFARIKI WAKIWA BADO NA UMRI MDOGO SANA!!

Image
RECHO: Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi ya mtoto wake aliyefariki muda mfupi baada ya kumzaa! RECHO: KUZALIWA 1988  KUFARIKI: 2014. UMRI: 26YRS KUAMBIANA: Hapa ndipo yalipo makazi ya milele ya Adam Kuambiana aliyefariki wiki iliyopita, leo akitimiza siku ya 13 kwenye makazi yake mapya  KUAMBIANA: KUZALIWA:  1976 - KUFARIKI: 2014  UMRI: 38Yrs JOHN MAGANGA: Haya ni makazi ya John Maganga akiwa leo naye anatimiza mwaka mmoja na miezi 6 JOHN: KUZALIWA: 1988 KUFARIKI: 2012 UMRI: 24Yrs MALISA: Haya ni makazi ya milele ya msanii mwingine Malisa ambaye ameshatimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atutoke ZUHURA: KUZALIWA: 1974 KUFARIKI: 2013 UMRI: 39Yrs KANUMBA: Haya ni makazi ya milele ya Kanumba ambaye sasa ana mika 2 na miezi 2 KUZALIWA: 1984 KUFARIKI: 2012 UMRI: 28yrs Hakika vijana wengi hivi sasa wanaondoka duniani mapema mno, wakiwa na umri chini ya miaka 30 na

TUKIO ZIMA KATIKA PICHA: TAZAMA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO, KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
  Majeneza yenye miili ya Recho na mwanaye.   Miili ya Rachel Haule 'Recho' na mwanaye ikishushwa kwenye gari maalum baada ya kuwasili Viwanja vya Leaders ikitokea nyumbani Palestina, Dar tayari kwa kuagwa.   Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya mwili kuwasili Leaders.

WAZIRI DK. MUKANGARA AWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA HABARI , VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO BUNGENI

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi, 35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi.  Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari wakifuatilia Hotuba hiyo.  Baadhi ya wadau wa Habari akiwepo Mkurugenzi wa Kituo cha Redio 5 cha jijini Arusha Francis Robert (kushoto) akifuatilia hotuba hiyo bungeni mjini dodoma leo.  Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akifuatilia mjadala wa Bajeti bungeni mjini Dodoma.  Wadau mbalimbali wa sanaa, Michezo na Utamaduni walikuwepo.  Wasanii wakifuatilia mjadala wa bajeti Bungeni, mtaalm Dude na kule P Funks mwaandaaji wa muziki na pia msaani wa muziki.

RECHO HAULE APUMZISHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE, KINONDONI DAR

Image
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Nyerere akiweka shada la maua katika kaburi la Recho. Ndugu wa marehemu wakiweka mashada. Wasanii wa Bongo Muvi kutoka kushoto Aunt Lulu akiwa na wenzake. Watumishi wa Mungu (katikati) wakifanya maombi baada ya maziko. Mchumba wa marehemu George Saguda (kushoto) akiweka udongo katika kaburi la Rachel na mwanae. Msanii Blandina Chagula 'Johari' akiweka udongo kaburini. Mjomba wa marehemu, Evance Haule (kushoto) akiweka udongo katika kaburi la marehemu. Ndugu wa marehemu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Rachel Haule. Mafundi wakichanganya zege. Mafundi wakisawazisha zege. (PICHA NA RICHARD BUKOS, DENIS MTIMA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHANI, HAMIDA HASSAN, IMELDA TARIMO/GPL)