Posts

MTOTO AZALIWA AKIWA NA VIDOLE 34..AVUNJA RECORD YA DUNIA

Image
The Indian boy broke the world record after being born with 34 fingers and toes. Akshat Saxena had seven fingers on each hand and ten toes on each foot, according to a spokesman for Guinness World Records. The child, from Uttar Pradesh in northern India, has since had a series of surgeries to amputate the excess digits. Akshat was born in 2010 without thumbs so doctors are working to reconstruct these out of the fingers they have removed. His mother Amrita Saxena said: "I was so happy to see my baby as it was our first child. "But later, when I saw his fingers, I was shocked and surprised." The condition is known as polydactyly, a genetic disorder which can be inherited and gives rise to excess digits. Most commonly, the extra digits appear on the little finger side of the hand. Mrs Saxena said it was a family friend who convinced them Akshat was extremely special. She said: "He read on the internet about the baby born in Ch

HIKI NDICHO KILICHOMKUTA MWANADADA WEMA SEPETU, MAHAKAMA YAAMURU KUNYANG'ANYWA GARI LA KIFAHARI AINA YA AUDI Q-7,

Image
  WEMA SEPETU  YAMETIMIA ! Ni kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha! Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu aliyesifika kwa kumwaga fedha kila kukicha ameanza kufilisiwa, Ijumaa Wikienda lina habari ya kipekee kuhusu mrembo huyo. Wema Isaac Sepetu. MAHAKAMA YAANZA Achilia mbali watu binafsi wanaochukua vyao baada ya mambo kuzidi kumwendea ndivyo sivyo, habari ya uhakika ni kwamba Mahakama ya Ilala, Dar imeridhia kukamatwa kwa lile gari lake la kifahari aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ lililokuwa likiwakosesha akina dada usingizi na kukabidhiwa kwa mmiliki halali kwa kuwa Wema alikuwa nalo kimagumashi. Gari aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ alilokuwa akiendesha Wema. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoenda shule vya Ijumaa Wikienda, gari hilo lilikamatwa Januari 2, mwaka huu Namanga, Oysterbay jijini Dar likiwa mikononi mwa kijana wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mdogo wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZIKO YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DK MGIMWA LEO IRINGA

Image
Mjane  wa Dr Mgimwa akiaga  mwili  huo kabla ya mazishi kijiji   cha Magunga  Iringa  leo  Mwili  wa Dr Mgimwa ukishushwa kaburini  leo  Wabunge  Deo  Sanga  wa jimbo la Njombe Kaskazin  kushoto na Deo Filikunjombe wa Ludewa   rais  Kikwete na mkewe  wakiweka  shada la maua  MAELFU   ya  wakazi  wa mkoa  wa Iringa na  baadhi  ya  viongozi  wa  vyama  vya  siasa na  Serikali  wakiongozwa na  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  wameshiriki  katika mazishi ya  aliyekuwa  mbunge wa   jimbo la Kalenga na  waziri wa fedha  Dr  Wiliam Mgimwa. Huku   waziri  mkuu Mizengo  pinda katika  salam  zake za serikali akielezea  jinsi ambavyo  Taifa  lilivyopata  pigo kubwa  kufuatia  kifo  cha Dr Mgimwa kutokana na mchango  wake  katika baraza la mawaziri. Katika  mazishi  hayo   yaliyofanyika  leo kijiji  kwake Magunga  jimbo la Kalenga   wananchi   mbali  mbali   walionyesha  kujipanga  barabarani  kutoka Manispaa ya  Iringa  hadi  kijijini kwak

TASWIRA YA MATUKIO WAKATI WA KUSIKILIZWA PINGAMIZI LA ZITTO KABWE MAHAKAMA KUU JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Dar es Salaam, SACP Marietha Minangi, wakati akiwasili Viwanja vya Mahakama Kuu.  Mmoja wa kijana aliyekamatwa na askari baada ya kuleta fujo eneo la mahakama.  Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo wananchi eneo la Mahakama Kuu.  Wafuasi wa Zitto Kabwe.  Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwahutubia wananchi waliofika mahakamani hapo baada ya hukumu ya Zitto kuahirishwa mpaka kesho saa nane mchana..  Wanausalama wakipanga mikakati ya kuimarisha ulinzi eneo la Mahakama Kuu jijini Dar.  Polisi wenye mbwa wakipita eneo la mahakama kuimarisha ulinzi.  Mmoja wa wafuasi wa Zitto akiwa na bendera.  Mwanasheria wa Zitto Kabwe, Albert Msando (kushoto) akitoka mahakamani baada ya hukumu kuahirishwa.  Wanahabari wakitoka eneo la mahakama. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutojadili uanachama

BELINA NAYE PIA AJIFUNGUA

Image
Belina Mgeni. MWANAMITINDO maarafu Bongo, Belina Mgeni amejifungua mtoto wa kike. Mtoto wa Belina. Mrembo huyo alijifungua juzikati katika Hospitali ya TMJ, iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam ambapo mwanamitindo huyo hakusita kuanika furaha yake mbele ya paparazi wetu kisha akatangaza jina la kichanga hicho, Naila. “Kiukweli siku zote ukimuomba Mungu unafanikiwa kwani nilikuwa naomba sana nipate mtoto wa kike na kweli imekuwa, namshukuru Mungu jamani,” alisema Belina pasipo kumuanika baba wa mtoto huyo.

MHUBIRI AFA MAJI BAADA YA KUJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU

Image
Iikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani. Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake. Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi. Tukio Hili la kusikitisha limetokea Huko Nigeria.

RAY C: NATESEKA KUISHI BILA MPENZI JAMANI

Image
STAA aliyebeba ‘taito’ kubwa ndani ya Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’  ambaye alitopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kisha kuyaacha, amefunguka kuwa yupo fiti na anataka kuishi na mpenzi, hayupo tayari kuteseka. Ray C. Ray C alifunguka hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram hivi karibuni ambapo bila hiyana alishindwa kuzuia hisia zake kama binadamu, akasema anatamani sana kupata mume anayempenda ili azae naye watoto wawili. Ray C ambaye hivi sasa yupo mstari wa mbele katika harakati za kupiga vita madawa ya kulevya, alisema anatamani kuwa na mume kwa sababu hataki familia ya mzazi mmoja kulea watoto kama alivyolelewa yeye na mama pekee. “Mimi nimelelewa na mama tu, malezi hayo siyo mazuri kabisa. Sipendi yatokee kwa wanangu ndiyo maana natamani nimpate mtu ambaye ananipenda kutoka moyoni, tufunge ndoa kabla ya kuzaa,” alisema Ray C. Baada ya mwanamuziki huyo kuandika ujumbe huo mtandaoni, walijitokeza wadau wengi ambao walikuwa

KAMA KITANDANI NI ZIRO (0), BASI HATA UWE MZURI VIPI NI KAZI BURE TU,,!!SOMA HAPA KUJUA MAUTUNDU

Image
Ni wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida. Mimi mzima na bado naendelea kuzungumzia mapenzi, mapenzi haya haya ambayo yamekuwa yakiwaliza baadhi ya watu kila kukicha. Wapo wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa katika uhusiano wao. Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya faragha ni moja wapo. Wapo wasichana au niseme wanawake ambao kimaumbile wana mvuto sana. Wamejaaliwa uzuri wa sura na kila kitu kiasi cha kutamaniwa na kila mwanaume wanayekutana naye. Lakini linapozungumziwa suala la mapenzi kwa mwanamke, wanaume wanaangalia vitu vingi, achilia mbali hilo la muonenako, pia wanaangalia utundu na ubunifu wa faragha. Hapo ndipo panapowakosesha raha b

KAJALA AFUNGUKA LIVE :NILIKAA DAWATI MOJA NA WATOTO WA RAIS JK

Image
Na Imelda Mtema HII ni safu mpya ambayo itakuwa ikizungumzia juu ya maisha ya kweli ya mtu yeyote maarufu. Itatokana na mahojiano ya ana kwa ana! Kwa kuanzia, tunaye nyota wa filamu za hapa nyumbani, Kajala Masanja, ambaye kabla ya kujiingiza kwenye sanaa hiyo aliwahi kuishi kinyumba na mmiliki wa studio ya Bongo Records, Paul Matheas, maarufu kama P.Funk na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Paula. Katika safu hii, Kajala ambaye amewahi kukutwa na misukosuko lukuki ikiwemo kuhukumiwa kifungo jela, anaelezea mambo mengi kuhusiana na maisha yake ambayo hakuwahi kuyaelezea kokote kule au katika chombo chochote cha habari. “Nilizaliwa mwaka 1983 katika familia ya mzee Masanja na walijaaliwa kuwa na watoto wawili tu, mimi na mdogo wangu, Dorice. Sisi tuna tofauti kubwa sana ya umri kati yetu kwa vile tulipishana sana kuzaliwa. Wakati nikizaliwa, wazazi wangu ambao wote ni askari polisi, walikuwa wakifanya kazi na kuishi kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam. “Kutokana