Posts

TAARIFA KAMILI JUU YA KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA "WILLIAM MGIMWA" HII HAPA

Image
:  Waziri wa Fedha William Mgimwa amefariki dunia leo katika hospitali ya Mediclinic Kloff nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa 6:20 kwa majira ya Tanzania

JOYCE KIRIA AFICHUA SIRI ZA NDOA ZAKE MBILI

Image
Ndoa ya pili ya Joyce Kiria na Henry Kilewo. Na Mwandishi Wetu MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel 5, Joyce Kiria amefunguka na kufichua siri ya ndoa zake mbili alizofunga, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili. Ndoa ya kwanza ya Joyce na DJ Nelly. Kwa mujibu wa mtandoa mmoja wa kijamii, Joyce alisema kwamba ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Nelson Nkongo ‘DJ Nelly’ walichangisha watu ili kufanikisha ndoa hiyo. “Kama desturi na utamaduni wetu tulichangisha lakini pamoja na michango mingi, tuliingia gharama zetu na kama haitoshi tulikopa na baada ya shughuli tulianza kupiga miayo ya njaa, hatukuwa na fedha tena na madeni yakatuandama,” alisema Joyce. Joyce na Kilewo siku ya ndoa yao. Mtangazaji huyo wa Kipindi cha Wanawake Live alisema kwamba alijuta sana lakini ikafika hatua ndoa hiyo ikasambaratika. Akiizungumzia ndoa yake ya pili na Henry Kilewo, ambayo awali ilifungwa Bomani, Joyce alisema kwamba haikuwa na makeke na wala kuchangisha watu fedha.

ANGALIA PICHA YA AJALI MBAYA IRINGA NI DAKIKA 20 BAADA YA MWAKA MPYA

Image
Hii ni ajali mbaya ya  piki piki iliyotokea  eneo la  Ilala katika Manispaa ya  Iringa  ikiwa ni dakika 20 baada ya  kuaga mwaka  2013 na kuukaribisha  mwaka  2014 ANGALIA PICHA ZAIDI

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA RAISI WA ZANZIBAR DK SHEIN

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa salamu za mwaka mpya wa 2014 kwa wananchi wa Zanzibar,pia amewataka wananchi kudumisha Umoja na kulinda amani na Utulivu uliopo ,salamu hizo alizitoa leo Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu.)

HUYU NDO BINTI WA YULE MBUNGE SHAROBARO WA KENYA

Image

China handovers Certificate of Vehicles; offers Tanzania more interest-free loans

Image
Mr. John M. Haule, Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation and H.E. Dr. Lu Youqing, Ambassador of the People's Republic of China to the United Republic of Tanzania sign Handing Over Certificate of Vehicles donated by the Chinese Government. Permanent Secretary John Haule receives Handover Certificate of Vehicles from H.E. Dr. Lu Youqing. The Chinese Government had donated 91 vehicles to the Government of Tanzania, worth Tsh. 9,450,000,000 which are purported to used for transportation at the Julius Nyerere International Convention Centre (JNIC) and various Government institutions.    Permanent Secretary John Haule and H.E. Ambassador Dr. Lu Youqing cut ribbon to officiate the handover of vehicles ceremony. Limousine luxury buses donated by the Government of the People's Republic of China to the Tanzania Government. Some of the Drivers from the Ministry of Foreign Affairs.  Officials fr

HII SASA NI FUNGA MWAKA AKAA JUU YA MNARA AKIHITAJI KUMUONA RAIS

Image
  Wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa huyo.     Wananchi wakishuhudia tukio hilo la kufunga mwaka 2013.     Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.   Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha. Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi. Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi ashijirushe na kufanikiwa kushuka naye. (PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)