MWANAFUNZI WA MIAKA 13 AJIFUNGUA MTOTO WA MIEZI 6 AKIWA SEBULENI BILA KUJIJUA....
MSICHANA aliyejitambulisha kwa jina la Salma Hemedi (13) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Dar amejifungua maiti ya kichanga cha miezi 6 bila mwenyewe kujijua. Tukio hilo lilitokea Septemba 25, mwaka huu maeneo ya Ubungo National Housing jijini Dar ambapo asubuhi ya siku hiyo, Salma alilalamikia maumivu ya tumbo lake kiasi cha mama yake aliyejitambulisha kwa jina la Rahma Shabani kwenda kuomba msaada wa kitabibu. Mwanamke huyo alieleza kwamba baada ya kurudi ndani alikomuacha mwanaye, alimkuta akiwa amejifungua kichanga sebuleni, kitu ambacho hakukitarajia kwa kuwa alizoea kumnunulia vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi kila alipomlalamikia maumivu ya tumbo akijua yupo kwenye siku zake. Akiwa na manesi walioongozana naye, walimsaidia Salma huku kila mtu akiwa amepigwa na butwaa kwa kilichotokea kwani hakuna aliyekuwa anajua kama Salma alikuwa na ujauzito. Akiongea na waandishi wetu, Salma alisema alipewa ujauzito na mwanaume aliyemtaja kwa jina