Posts

BOKO HARAM Lavamia chuo cha kilimo na kuua WANACHUO 50 wakiwa wamelala

Image
Mamlaka nchini Nigeria zimesema kuwa hakukuwa na ulinzi katika chuo cha Kilimo ambako wanafunzi 50 waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa wamelala. Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya tukio hilo lililotekelezwa na wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislam wa kundi la Boko Haram katika chuo hicho katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Ofisa mmoja wa serikali amesema, serikali na jeshi la wataimarisha ulinzi kwenye maeneo ya shule na kuongeza kuwa licha ya shambulio hilo masomo yataendelea kama kawaida.

UPDATE"mbunge Godbless Lema afutiliwa kesi ya UCHOCHEZI iliyokuwa inamkabili "

Image
Kesi iliyokua inamkabili Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema dhidi ya Mkuu wa Mkoa kwa kusababisha fujo Chuo cha Uhasibu Arusha imefutiliwa mbali na Mahakama kuu muda huu. TUTAKUJUZA HABARI ZAIDI BAADAE .  

Mama ajifungua CHURA...Yadaiwa kuwa mbegu za uzazi wa chura alizipata akioga katika bwawa lenye vyura

Image
Mama mmoja nchini Kenya amejifungua mtoto wa ajabu ambaye anafanana na viumbe wawili wa dunia hii... Sehemu ya juu ya mtoto huyo inafana na chura huku sehemu ya chini ikifanana na binadamu wa kawaida.... Mtoto huyo ambaye alizaliwa wikiendi iliyopita anaonekana kutokuwa na shingo huku macho yake yakiwa kama ya chura. Ripoti ya kitaalamu toka hospitali ya Gaurishnkar ambako mtoto huyo alizaliwa imeeleza kuwa mama huyo aliingiliwa na mbegu za uzazi wa chura wakati akioga katika bwawa la maji.. "Tulifanya mazungungumzo na huyu mama na akatueleza kuwa alikuwa na mazoea ya kuoga katika bwawa.Tunaamini kwamba mbegu za chura zitakuwa zilimwingia wakati akiwa katika siku hatari"..Alisema dakatari mmoja

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI.... NI UKATILI WA AJABU KWA KICHANGA

Image
  Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo. Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa. Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo. Rukia Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Natafuta Mume wa NDOA....Nipo tayari kumpenda kwa dhati na SITAMSALITI.

Image
phars. Mimi ni binti mjasiliamali ambaye nimechoka kuishi peke yangu na sasa nahitaji mwanaume wa ndoa anayejiheshimu na anayejua kupenda.Umri wangu ni miaka 25, elimu yangu ni form six. Asilimia kubwa ya wanaume ni wasumbufu na wana wanawake wengi,kitu ambacho kwa upande wangu sikitaki maana najijua nina wivu.... Kwa yeyote mwenye sifa hasa ya kuja kuwa mume mwema ambaye atanipenda kwa dhati na hatanisaliti basi anijibu kupitia email yangu. Kwa upande wangu namhakikishia kuwa ntampenda kwa dhati, Sitamsaliti, ntamheshimu na ntawapenda ndugu na jamaa zake wote kwa moyo wangu wote. Mawasiliano: Email yangu ni nancybast4@yahoo.com   FURSA KWENU VIJANA MNAITAFUTA MCHUMBA

PICHA YETU YA LEO,"JE OFISI YAKO INA MUUNDO HUU"

Image
    FOR MORE INFORMATION LIKE OUR FACEBOOK PAGE

JE, ADHABU HII INASTAHILI KWA WATOTO?

Image
Serikali imekuwa ikipinga sana kutolewa kwa adhabu za viboko shuleni , lakini kila kunapokucha Walimu nao wanabadilisha mbinu za adhabu na kuamua kutoa adhabu kama hii kwa watoto kwa kuwalaza juani na kuwaacha hapo kwa muda pasipo kuchapwa viboko. Je,Ukiwa kama mdau wa Elimu unafikiri kutolewa kwa adhabu hizi ndio sitasaidia kukuza elimu yetu? TUPIA MAONI YAKO, NA PIA USISAHAU KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

THIS IS A MOST BEATIFUL IN THE WORLD 2013.

Image
( Miss World 2013 )....Ghana washika nafasi ya tatu Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo. Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana. Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo. MREMBO wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani mwaka huu (2013) juzi huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria kulivuruga tukio hilo. Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea". Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani t...

NORA AINGIA MATATANI MARA BAADA YA KUMCHAPA MAKOFI MHUDUMU WA HOTELI HUKO MABIBIO MARA BAADA YA KUGOMA KULIPA DENI LA TSHs. ELFU TATU...!!

Image
STAA wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘ Nora’ anadaiwa kumzaba makofi mhudumu wa Hoteli ya Lunch Time, Mabibo, Dar aliyetajwa kwa jina la Joyce Mashika. Joyce Mashika. Katika tukio hilo lililojiri wiki iliyopita hotelini hapo, ilidaiwa kuwa kisa cha yote hayo ni kufuatia Nora kudaiwa shilingi elfu tatu za Kitanzania, deni aliloliacha kwenye gharama ya hoteli ambapo alitakiwa kulipa shiling elfu 30. Joyce aliwaambia wanahabari wetu kuwa Nora alifika hotelini hapo, akaomba chumba na alipoambiwa atoe fedha kwanza aliomba udhamini aingie hotelini kisha atalipa mpenzi wake akifika. Joyce alidai kuwa walichukua muda wa nusu saa kukubaliana naye lakini baadaye walimpigia meneja wa hoteli ambaye alikubali Nora apewe chumba. Alidai kuwa alipofika mpenzi wake ambaye ni mtu mzima, Nora alilipa shilingi elfu 20 na kuacha deni la shilingi elfu 10 aliahidi kulipa wakati anatoka. Joyce alidai kuwa usiku Nora aliagiza chakula na wakati anakilipia akampa mhudumu shilingi elfu...

ROSE NDAUKA KUJIFUNGUA BILA NDOA

Image
phars Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. “Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye ...

LULU AWAONYESHA FURSA WAKAZI WA MWANZA

Image
phars  Msanii wa Filamu Bongo,Lulu akiongea jambo na wakazi wa Mwanza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa Golden Crista mapema hii Lulu akipokea pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Steven Masele muda mfupi baada ya kushuka jukwaani kuzungumzia mambo ya Kamata Fursa Twenzetu

PHARS NYANDA BLOGGER ATOA MSAADA WA VITABU KATIKA SHULE VIZIWI DONGOBESH...

Image
  Phars akikabidhi msaada wa vitabu hivyo mbele ya Mwalimu katikati na Mwalimu Mallya kwa niaba ya Walimu wengine . Ikiwa ni Wiki ya maadhimisho ya VIZIWI Tanzania .Phars Msirikale kupitia Phars blog imeamua kutembelea shule ya Msingi DONGOBESH VIZIWI iliyoko Mkoani Manyara Wilaya ya Mbulu na kutoa msaada wa Vitabu vya Kiada na Ziada vipatavyo 147 vyenye thamani Tsh. 876,000/= kama msaada kwa watotot hao . Phars blog inapenda kutoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kwasaidia watoto hao kwani wanayo mahitaji mbalimbali dhidi yao yanayowakabili.  The blogger akiwa na wanafunzi wakionesha vitabu ambavyo wamepelekewa kama msaada kwao  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Dongobesh Viziwi akiwa na wanafunzi wake mara baada yakupokea msaada wa vitabu  Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kutangaziwa kuna mgeni kafika nakuwaletea zawadi ya vitabu kama wanavyoonekana hapo.  Mwalimu Rose akiwa na Mwalimu mwenzake nae akiwa na wanafunzi wake wakiangalia...

Wanawake Elfu 8 nchini Nigeria waandamana kuishinikiza Serikali iwasaidie WAOLEWE

Image
je ingekuwa Tanzania ingekuwaje? Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua. Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa. Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!) Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine. Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao.

JINSI YA KUZUIA NA KUTIBU KUHARISHA WAKATI UNAPOKUWA SAFARINI

Image
  Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini? Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika sehemu hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa safari na kubadilisha chakula. Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na sababu nyingine? Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa, maumivu ya tumbo na kichefu chefu. Nitazuiaje kuharisha? Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula, pia mara nyingi kuo...

MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUPIZI HARAKA, NA KUSHINDWA KURUDIA RAUNDI YA PILI

Image
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume. Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani. Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili. Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi amba...

Ray C atamani penzi la MKENYA aliyejitosa na kuokoa mamia ya mateka wa Alshabaab

Image
Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita. Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto. “In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji. “I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine. Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.” Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ...