Posts
AISHA BUI AFUNGUKA JUU YA SHUTUMA ZA KUWA KAFUNGWA UKO BRAZIL
- Get link
- X
- Other Apps
HUKU kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na kufafanua juu ya tuhuma hizo. Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari kulianika. “Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu. “Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya. “Naomba Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha .
Rais Jakaya Kikwete atembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dkt Jakaya Kikwete akitembea kwa miguu kutoka hotelini kwake kuja kwenye Ubalozi wa Tanzania Marekani siku ya Jumatano Sept 18, 2013 na kukutana na Mabaozi wa Heshima ambao jana Jumatano wasaini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataofanyakazi wakiiitangaza Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya uwekezaji, Utalii na mambo mengine yatakayosaidia kuinua uchumi wa Tanzania. Rais Dkat Jakaya Kikwete akisalimiana na Maafisa Ubalozi wakiwemo wafanyakazi mara tu alipoingia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabra ya 22, Washington, DC Rais Dkt Jakaya Kikwete akitia saidi kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku Mhe. Waziri Bernard Membe na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakishuhudia. Raus Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama William alipokua akiingia chumba cha mikutano cha Nyerere Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana
HIVI NDIO OMMY DIMPOZ ALIVYOWASILI JIJI LA MARAHA, WASHINGTON DC
- Get link
- X
- Other Apps
ASEMA YUPOTAYARI KUACHA HISTORIA MAREKANI KUANZIA JUMAMOSI HII WASHINGTON DC ! OMMY DIMPOZ ALIPOWASILI WASHINGTON DC “OMMY DIMPOZ” AKIWA NA PROMOTER WAKE “DMK GLOBAL” DIMPOZ AKIPATA UKODAKI NA PROMOTER WAKE “MR DMK” PAMOJA NA AKINA DADA WALIOKUWEPO KUMPOKEA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA WASHINGTON DC.KULIA NI MLIMBWENDE ALIYEWAHI KUTWAA TAJI LA MISS TEMEKE NA KUSHOTO NI MLIMBWENDE MWINGINE KUTOKA TZ. OMMY NDANI YA LIMO KUELEKEA HILTON. LUNCH TIME AT THE HILTON. OMMY DIMPOZ AKIWA NA DESIGNER MISS TEMEKE NA GAUNI LAKE LA KWETU FASHION.
Messi amjibu Ronaldo, apiga hat trick, barca ikiua ajax 4-0
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji wa Baraca wakishangilia pointi tatu Lionel Messi akifunga bao Lionel Messiamejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp. Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique. Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson. Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69. Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
UNAFIKIRI VAZI HILI LINAFAA KUVALIWA WAPI NA WAKATI GANI?
- Get link
- X
- Other Apps
JOHARI AKIRI KUZICHAPA NA HANSI CHUU KISA PENZI LA RAY...HUU NDIO MKANDA MZIMA WATUKIO HILO
- Get link
- X
- Other Apps
Waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wanadaiwa kuchapana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent Kigosi ‘Ray’, TUHUMA Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu wa wasanii hao, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ofisi za RJ Productions, zinazomilikiwa kwa ubia wa Ray na Johari zilizopo Sinza-Mori jijini Dar ambapo Johari alikuwa akimtuhumu Chuchu mambo mazito ya kimapenzi kwa Ray. Shushushu huyo alitonya kuwa, siku ya tukio Johari na wasanii wenzake walikuwa wakirekodi filamu ndani ya hoteli moja (jina tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo ndipo alipofikishiwa umbeya kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi hizo ‘akijiachia’ na bosi mwenzake (Ray), jambo lililotia ganzi moyoni mwa mdada huyo. MCHEZO MZIMA ‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kuwa baada ya Johari kupata habari hizo, bila kujiuliza wala kuvuta subira, ‘alisaga soli’ hadi maeneo hayo. “Alipofika a
SHAHIDI AFARIKI GHAFLA MAHAKAMANI WAKATI AKITOA USHAHIDI HUKO MKOANI MARA...!!
- Get link
- X
- Other Apps
Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati, wilayani Rorya, mkoani Mara, Charles Warito (38), ambaye ni shahidi wa mlalamikaji katika Kesi ya kudhuru mwili kwa kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kusababisha ulemavu amefariki dunia, wakati akitoa ushahidi. Warito alikutwa na umauti huo akiwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime mbele ya Jaji G. Ndika anayesikiliza kesi katika Wilaya za Tarime na Rorya. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana mchana baada ya Mwanasheria wa Serikali, Mayega na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta George Lutonja walimwita kuingia Kizimbani tayari kutoa ushahidi. Shahidi huyo alianza kutoa ushahidi wake na alieleza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na mtuhumiwa Kichohe Kichere ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Omoche Kata hiyo ya Nyahongo Shirati Januari 26, mwaka 2008 na kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kukatwa mkono na mwili wake ulianza kupooza na kulemaa up
RIPOTI YA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNESS MASOGANGE NA MELLISA
- Get link
- X
- Other Apps
WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa. Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya. Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8. Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza
ANGALIA PICHA YA DENTI WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU NA KUWEKA SEHEMU ZA SIRI.
- Get link
- X
- Other Apps
Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry. Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na ndipo watu walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga
Mbwa waliotumika kumlinda Prince William jeshini wauawa
- Get link
- X
- Other Apps
-Kwa sababu ya kushidwa kupangiwa majukumu mapya au kupelekwa nyumbani kwa mwana mfalme Mbwa wawili walinzi wa Prince William wa Uingereza wameharibiwa na kuondolewa katika viwanja vya kifalme vya ndege za kivita wakati Prince huyo ambaye alikuwa akifanya kazi ya kijeshi ya anga baada ya kushidwa kupangiwa kazi zingine mbwa hao waliteketezwa siku chache kabla ya mwana wa mfalme kuondoka. Prince William ambaye amepata mtoto hivi karibuni alikuwa katika majukumu yake ya kijeshi na mazoezi ya utafutaji na uokoaji katika eneo la kijeshi la North Wales wiki iliyopita. Ndani ya siku moja baada ya kuhama, walinzi wake mbwa wawili waliharibiwa kabisa siku ya Ijumaa wiki iliyopita. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Uingereza amesema mbwa hao aina ya shepherd Brus toka Ubelgiji na Ujerumani walikuwa wameezeka na hawakuweza kupangiwa majukumu mengine.
ANGALIA PICHA ZA PICHA MAMBA ALIVYO ZUA BALAA BAADA YA KUINGIA CHINI YA KITANDA HOTELINI
- Get link
- X
- Other Apps
Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8. Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata. Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo. Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe
SEREKALI KUMLIMA BARUA BALOZI WA CHINI BAADA YA KUJIHUSISHA NA CCM
- Get link
- X
- Other Apps
Dar es Salaam. Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za diplomasia. Pia, inasema inajiandaa kumwandikia barua Balozi wa China nchini, Lu Younqing kutokana na hatua yake ya kujihusisha na mambo ya siasa. Wiki iliyopita, Balozi Lu alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mkoani Shinyanga, huku akiwa amevalia moja ya sare za chama hicho, hatua ambayo imezusha mjadala miongoni mwa vyama vya siasa na wachunguzi wa mambo ya kidiplomasia. Akizungumzia kitendo hicho jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema Serikali inajiandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa zake. Hata hivyo, Mahadhi alisema Tanzania na China zitaendelea kuwa marafiki wanaoshirikiana kwenye nyanja mbalimbali kw
Waliolipua mabomu katika mkutano wa CHADEMA jijini Arusha wakamatwa
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo. WATUHUMIWA walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenyemkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema hayo jana katika mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti. “Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani." Mulongo alisema kwa sasa Polisi iko katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo. Malengo mengine kwa mujibu wa Mulongo ni kuwafahamu watu wote waliopewa zabuni ya
Pesa zazidi kumwagika kwa DIAMOND...Haya ni mamilioni aliyopewa na VODACOM
- Get link
- X
- Other Apps
Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, punde baada ya kusaini mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh 50,000 kwa siku. Anayeshuhudia ni Salum Mwalim, Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania. Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (mwenye fulana nyekundu) akiucheza wimbo wake mpya ujulikanao kama My Number One, wakati wa uzinduzi wa mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo huo kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh 50,000 kwa siku. Mkataba huo ni baina ya Diamond Platinumz na Vodacom Tanzania. Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitia ofa hiyo, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama