Messi amjibu Ronaldo, apiga hat trick, barca ikiua ajax 4-0


mess2 79190
Wachezaji wa Baraca wakishangilia pointi tatu

messi 3a3f5
Lionel Messi akifunga bao
Lionel Messiamejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.
Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.
Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen. 

Katika michezo mingine matokeo ni 

Schalke 3-0 Steaua

Milan 2-0 Celtic

Atlético 3-1 Zenit

Austria Wien 0-1 Porto

Chelsea 1-2 Basel

Marseille 1-2 Arsenal

Napoli 2-1 Dortmund

 Chanzo: binzubeiry

Comments

Popular posts from this blog