Posts

BREAKING NEWS: NDEGE ZAGONGANA ZANZIBAR.

Image
Ndege ya Oman air na Ethipian airlines leo jioni zimegongana katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar wakati zikijitaarisha kuruka, ila ajali hii haikuwa kubwa, wakati hayo yakiendelea abiria wa Ehiopian airline wameshushwa na kuweka sehemu ya mapumziko. Nawatakia kila la kheri wasafiri wote na inshaalah Mwenyezi  Mungu atawapa wepesi wa katika safari zao. Ndege ya kulia ni ya Ethiopian airlines mayo ndiyo imeivaa Oman air hadi bawa kutoka source http://www.jestina-george.com

PICHA; YALIYOJIRI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA...!!

Image
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika kumuanga SHUJAA WA INJILI Dr Moses Kulola aliyefariki 29 Agosti saa 5.30 hapa jiji Dar. Kati ya watu ambao wamekuwepo katika ibada hii ya kuuaga mwili wa Dr Askofu Moses Kuloa, wamehuduria watumishi wa Mungu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maaskofu wainjilisti mitume na manabii. Askofu kulola alizaliwa mkoani Mwanza, mwaka 1930 na kufariki 29 agost 2013. Baadhi ya watumishi Katika uhai wake mzee Kulola alifanya kazi ya Injili hadi kifo kinamchukuwa, ila kati ya kazi aliyoifanya ni pamoja na kutembea kwa mguu kutoka Mza hadi Mtwara. Lakini pia safari nyingi alizozifanya zilikuwa katika mazingira magumu. Amehubiri injili ndani na nje ya nchi. Mama Kulola (Mjane Mtoto wa Mzee Kulola Willy, akilia kwa uchungu   Askofu Silvester Gamanywa akimpa pole mama Kulola Watumishi wa Mungu mbalimbali wakisubiria mwili wa Dr Moses Kulola Msafara wa mwili wa marehe...

SISTER FEKI ANASWA NCHINI KENYA

Image
Sister feki baada ya kunaswa akikusanya fedha. ..Akipekuliwa mabegi… POLISI mjini Narok nchini Kenya wanamshikiria mwanamke mmoja aliyenaswa akiwa na mavazi ya kitawa akikusanya fedha kutoka kwa watu wenye mapenzi mema akidanganya kuwa ni sister. Mwanamke huyo alikuwa akikusanya misaada ili aweze kurudi katika konventi alipotokea mpaka hapo aliposhutukiwa kuwa hakuwa mtawa. Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitambulisho kadhaa. Mpaka ananaswa, sister huyo alikuwa amewatapeli watu kadhaa na anatarajiwa kufikishwa mbele ya sheria kesho.  Habari / Picha: KTN

Obama ataka bunge liamue kuhusu Syria;

Image
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa , Ikulu ya Marekani ya White House imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria. Lakini hayo yamebadilika rais Obama anataka sasa bunge liamue. Uamuzi wa Rais Barack Obama wa ghafla badala yake wa kuomba ruhusa ya bunge unamuweka katika hatari ambayo inaweza kuharibu hali yake ya kuaminika iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa kujibu shambulio la silaha za kemikali ambalo limekiuka kile binafsi alichosema kuwa ni kuvuka "mstari mwekundu". Bunge la Marekani halijatatua karibu chochote cha maana tangu mwaka 2010, likishindwa kukamilisha kile ambacho hapo kabla kilikuwa wajibu wa msingi kwa masuala ya barabara , shule , mashamba na masuala ya mawasiliano nchini Marekani. Kuomba ruhusa ya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican pamoja na baraza la seneti linalodhibitiwa na chama chak...

MWANAMKE HUYU ADHAMIRIA KUWEKA REKODI YA DUNIA KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAUME 100,000 DUNIANI KOTE....!!

Image
Mwanamke mmoja raia wa Poland ameripotiwa kuweka nadhiri ya kusafiri katika kila mji duniani katika uchunguzi usio wa kawaida kulala na wanaume 100,000. Ania Lisewska kutoka mjini Warsaw ameingia katika mpango huo usio wa kawaida kwenye mji aliozaliwa mwezi uliopita na mpaka sasa amefanikiwa kuongeza idadi hiyo kufikia 284, kwa mujibu wa gazeti la Huffington Post. Lakini wakati rafiki yake wa kiume wa muda mrefu mwenye umri wa miaka 21 akimsamehe zaidi kuliko wote - hajamtosa pamoja na yote hayo - anaeleweka kwamba 'hajasisimuliwa' na wazo hilo. Ania alisema kwamba rafiki yake huyo amelazimika 'kukubaliana na wazo hilo'. Alilieleza gazeti la Austrian Times: "Nataka wanaume kutoka Poland, Europe na duniani kote. Ninapenda ngono, kufurahi na wanaume. "Nchini Poland somo la ngono bado ni haramu na yeyote anayetaka kukidhi matakwa yao ya ngono huchukuliwa kama aliyepotoka, au mgonjwa wa akili....

MAMBO YAKUZINGATIA KWA WANAWAKE WANAO TAKA KUOLEWA

Image
Hata kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo. Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke  anasubiri kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake. Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika. Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kw...

UVCCM LAMUIDHINI​SHA SIXTUS MAPUNDA KUWA KATIBU MKUU MPYA

Image
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akifungua Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Zanzibar), Shaka Abdul Shaka, Katibu Mkuu wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Martine Shigela na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

Mwili wa Askari aliyefariki kwenye Mapigano Congo Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo Wawasili nakuzikwa Zanzibar.

Image
Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.  Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam.  Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika na Ndugu na Jamaa kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo.ulipowasili Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa mazishi jioni hii.  Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba ya kuupokea Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja wa ndege wa Zanziba leo mchana na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.  Mjane wa Marehemu na Watoto wake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume leo mchana wakitokea Mjini Dar-es- Salaam.  WANAJESHI wa Jeshi la Wananc...

MCHUNGAJI ATOA SIRI ALIVYOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA

Image
  Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kipendekoste la Kiinjili Tanzania, kwenye ofisi za gazeti hili wakati akitoa ushuhuda wa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Kinara wa kimataifa wa kuuza madawa ya kulevya aliyezunguka sehemu mbalimbali duniani kuuza mihadarati, ameacha biashara hiyo na sasa anahubiri Injili kupiga vita dawa hizo. Kigogo huyo Mtanzania na mzaliwa wa Mbeya, ambaye sasa anajiita kiumbe kipya katika Kristo, ni Mchungaji Macdonald Mwakisambwe wa Kanisa la Kipentekoste la Kiinjili jijini Dar es Salaam.   Akizungumza katika mahojiano maalumu  Jumamosi jana, Mwakisambwe alisema alianza biashara ya unga mwaka 1990 na kuifanya kwa miaka 10, akisafirisha dawa kwa maelfu ya wateja walioko Afrika, Asia, Ulaya na Amerika. Alisema katika kutimiza azma hiyo, alitumia pasi za kusafiria za mataifa mbalimbali zenye majina tofauti, zikimuonyesha kuwa ni raia wa Msumbiji, Tanzania, Kenya, Namibia, Afrika K...

Kili Music Tour 2013 Yapagawisha Kigoma, Tazama picha za matukio kamili.

Image
  Ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu imefanyika mkoani Kigoma na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika uwanja wa Lake Tanganyika baada ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo ya jirani kufurika kwa wingi kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda jukwaani. Kivutio kikubwa katika tamasha hilo ilikuwa ni wanamuziki wanne wanaounda kundi la Kigoma All Stars, Diamond, Mwasiti, Linex na Recho kupanda mwishoni na kuimba wimbo wao maarufu wa Leka Dutigite na kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyotokea.