HIKI NDO KICHAPO WANACHOPEWA WAASI WA M23 NA JESHI LA KONGO ( FARDC )
Goma -DRC. WAKATI mapigano yakizidi kuwa makali kati ya wanajeshi wa DR Congo (FARDC) na kundi la waasi wa M23, wanajeshi wa DRC wako hatarani kushitakiwa kwa tuhuma za kuwatesa waasi na kunajisi maiti zao. Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kosa la kukiuka haki za binadamu na sheria za Umoja wa Matifa (UN) inayokataza ukiukwaji wa haki za binadamu huku ukikataza watuhumiwa na mateka wa kivita kufanyiwa vitendo vyovyote vinavyo ashiria kukiuka haki zabinadamu badala yake mateka wote wanatakiwa kushtakiwa kwa muujibu wa sheria. Maiti ya muasi wa M23 ikinajisiwa na Askari wa Congo,baada ya kukamatwa, kuteswa hadi kufa katika mapigakano yanayoendelea maeneo ya Kivu na Goma nchini Congo. Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon alisema kwamba, Umoja huo umeonyesha wasiwasi kuhusu taarifa ya kutokutendewa haki kwa wafungwa wa M23 na kunajisiwa kwa maiti ya wapiganaji wa M23 baada ya kukamatwa na vikosi vya silaha. Alisema watuhumiwa wa M23 walifanyiwa vit