MAUAJI YA WANAJESHI DARFUR, HOFU YATANDA


Mmoja wa majeruhi katika shambulio la wanajeshi huko Darfur nchini Sudan.
Na Mwandishi Wetu

KUFUATIA kushambuliwa na kuuawa kwa wanajeshi saba wa Tanzania huko Darfur nchini Sudan, hofu imetanda kwa ndugu na jamaa wa askari mbalimbali walio nje ya nchi yetu.
Wakizungumza juzi katika ofisi zetu Bamaga, Mwenge  Dar kwa nyakati tofauti huku wakiomba kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya ndugu wa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) walio katika kazi maalum ya kulinda amani huko Darfur, DR Congo na Lebanon wamesema hofu yao inakuja baada ya kusikia kuwa huwa hawatumii silaha kujilinda.
Gari la wanajeshi walioshambuliwa.
“Sasa kama hawatumii silaha na wanatumia virungu na wenzao wanatumia bunduki tena za kisasa hofu yetu ni kwamba watazidi kushambuliwa na kuuawa,” alisema ndugu mmoja. NA GLOBAL PUBLISHER
Ndugu mwingine alisema kwamba wanakuwa na wasiwasi mkubwa na kutaharuki kutokana na maelezo yanayotolewa kupitia vyombo vya habari vya nje kwamba Congo na Darfur mapambano hivi sasa yamepamba moto.

Moja ya jeneza lenye mwili wa mwanajeshi likiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kusafirishwa.
“Kama mapambano yamepamba moto, hawa ndugu zetu watajihami kwa sialaha gani? Tunaiomba serikali ifanya kila linalowezekana ili askari wetu warudishwe nchini,” alisema jamaa mwingine aliyesema yeye kaka yake yupo DR Congo.
Baadhi ya majeruhi wa shambulio hilo wakiwa hospitali.
Majeshi hayo ya Tanzania yanalinda amani katika nchi za DR Congo, Darfur na Lebanon chini ya mkataba wa Azimio la Umoja wa Mataifa  Nambari 2098  la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Comments

Popular posts from this blog