Posts

RAIS KIKWETE AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JWTZ CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI, LEO

Image
   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali V.K. Mritaba. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  gwaride katika  Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo. ZAIDI BOFYA HAPO CHINI   Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpa zawadi  Ofisa Kadet  Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Mondu...

RAY C AZIDI KUPENDEZA, MASHABIKI WAZIDI KUMSHANGAA..

Image
Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka. Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake. Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka. UNENE UNATOKANA NA DOZI? Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’. Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga. AFUT...

PICHA MBALI MBALI ZA KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA WA MAMA YAKE PROF J MBEZI YA KIMARA

Image
dolo na nature Juma nature akimpa pole prof j NA  http://phars.blogspot.com/

"RED BRIGED NI LAZIMA IANZISHWE...MBONA CCM NA CUF WANA KUNDI LAO?"...CHADEMA

Image
  SINGO BENSON Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitarudi nyuma katika mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu kupitia kikundi chake cha red brigade. Chama hicho kimesema, tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), vyote vikiwa miongoni mwa `vyama vikubwa nchini’, vina vikundi vya aina hiyo.   Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo Chadema, Singo Benson, ametoa msimamo huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. Tamko la Chadema kuanzisha mafunzo hayo, limeibua taharuki na kusababisha watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutaka mpango huo usitishwe. LENGO LA MAFUNZO Benson alisema lengo la kuimarisha kikundi hicho, ni kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wake, ambapo CCM ikitajwa kuwa nyuma ya mashambulizi hayo. Alisema Chadema, imekamilisha maandalizi ya mafunzo yatakayowajumuisha zaidi vijana, ili wapate mbinu za kujiking...

MPENZI WA NAY WA MITEGO AIPOTEZA MIMBA YAKE BAADA YA KUANGUKA

Image
Rapper Nay wa Mitego leo anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mchumba wake aliyekuwa mjamzito kwa huzuni kubwa baada ya mchumba wake huyo kukipoteza kichanga chao kufuatia kuanguka jana usiku. “Jana usiku mke wangu alianguka, alifikia tumbo kwahiyo akawa anasikia kizunguzungu nilipompeleka hospitali daktari akasema mtoto amekufa,” Nay . Awali, Nay wa Mitego ameweka picha ya mchumba wake kwenye Instagram akiwa hospitali na kuandika:  Happy bday my lv, Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio tele. Japo imekukuta uko vibaya tumempoteza kijacho bt ni mipango ya mungu, nakupenda sana mke..!! #966# happy bday 2u ma.”

HIKI NDO KIASI CHA PESA ANACHO INGIZA RAISI OBAMA KWA MWAKA

BAADA ya kuchaguliwa katika awamu ya pili ya utawala wa Marekani, Rais Barack Obama, ameendelea kupata mshahara wa dola 400,000 kwa mwaka. Wakati alipopata utawala, Rais huyo mwenye nguvu duniani ameendelea kuwa Kamanda wa Jeshi la Marekani, Rais mwenye nguvu duniani na ameendeleza utawala wa Air Force One. Obama alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza, kipato chake kilikuwa dola 1.3 milioni. Miaka minne baada ya kukaa Ikulu kipato chake kimeongezeka kwa asilimia 800 sasa anapata dola 11.8 milioni. Kipato kimeongezeka vipi? Awali Obama alikuwa na kipato kidogo, alikuwa akilipwa dola 60,000 kwa mwaka alipokuwa Seneta wa Illinois na baadaye akawa analipwa dola 175,000 kwa mwaka. Jambo la kufurahisha ni kuwa kabla Obama hajawa Rais, hakuwa na mshahara mkubwa, hata mke wake, Michelle,  alimzidi kwa kipato. Michelle alikuwa akiingiza kiasi cha dola 320,000 kwa mwaka, wakati huo alikuwa Makamu wa Rais wa Kitengo cha U...

MAANDAMANO MAKUBWA TOKA MISRI YAFANYIKA LEO

Image
Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi Wanafanya maandamano makubwa mjini Cairo mchana huu, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadan. Wafuasi wa Bwana Morsi wanatarajia kuwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo, wataendelea kuunga mkono wito wao wa kutaka Bwana Morsi kurejeshwa madarakani. Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir. Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa. Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa. Marekani kutuma ndege za kivita Misri Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za...

MAISHA BORA KWA MTANZANIA JE YANAKIDHI.......

Image
Hawa ni vijana kutoka MKOANI - MANYARA maeneo ya HARKA waliokutwa wakijadilini ni kwa jinsi gani wapataweza kupata unga angalau hata robo kilo ili wakapike kupunguza ukali wa njaa mara baada yakupata mboga mafungu mawili ya mboga za majani,na hatimaye msamaria mmoja kuhamua kuwanunulia mua ili wapunguze njaa zao. Ukiwa kama Mtanzania Mwenzetu je ungewasaidiaje hawa vijana. TUPE MAONI YAKO

HUYU ndo MWANAJESHI ALIYEKAMATWA NA JINO LA TEMBO ANGALIA PICHA

Image
Mwanajeshi anayesadikiwa kukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake, huyu alitegemewa kuilinda Nchi lakini . (Picha na maktaba) Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3. Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka. Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi. Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye t...

KILA SIKU KUNA JIPYA MZEE ASEMA ANATAKA KUMFUFUA NYERERE

Image
MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.   Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM, anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia! Madai yake mzee huyu anasema anaenda kumfufuana Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.

TANZANIA YAMJIBU RAIS KAGAME....YADAI IPO TAYARI KWA LOLOTE NA AKITHUBUTU ITAMCHAPA KAMA MTOTO

Image
SERIKALI ya T anzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza. Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania. Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame. Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesa...

HALI ILIVYO NYUMBANI KWA PROF JAY

Image
Huyu ni mtoto wa Prof Jay anaitwa LISA ndio ameingia nyumbani hapa kwenye msiba wa bibi yake kipenzi Hali ilivyo asubuhi hii hapa nyumbani kwa Prof Jay ambapo ndipo ulipo msiba wa mama yetu.. kwa wanaotaka kuja msiba upo Mbezi mwisho baada ya stendi mpya ya mabasi basi mbele kidogo mkono wako wa kushoto utaingia utaona nyumba kumba ipo kwa chini na magari mengi basi ndio hapo hapo. Kwa wanaokuja na daladala baada yakupita hiyo stendi mpya utamwambia konda akushushe kwa Prof Jay maana ndio kituo hicho. RIP MAMA MAJANJALA Pichani ni wasanii wa bongo fleva wakiacha kumbukumbu katika kitabu cha maombolezo. Kushoto ni Dullayo pamoja na mdogo wake Prof Jay anaitwa Black Rhino mwenye tshirt ya kijani   KWA HISANI YA DJ CHOKA

MATUKIO YA PICHA YALIYOJIRI KWENYE MSIBAA WA MAMA YAKE Z ANTO

Image
Matukio mbalimbali yaliyoweza kutokea uko nyumbani kwenye msiba wa mama yake Z anto NA  BONGO CLAN

ANGALIA PICHA MATUKIO YANAYOENDELEA KWENYE MSIBA WA MAMA YAKE PROF J

Image
PICHA NA  http://djchoka.blogspot.com

PREZZO AMPONDA DIAMOND....

Image
Majigambo ya Diamond kwenye vyombo vya habari kabla ya Tamasha la Matumaini kufanyika kuhusu kumgalagaza Prezzo kwenye show hiyo hayajampendeza Rapcellency na sasa ameamua kujibu. Prezzo ambaye jina lake halisi ni Jackson Makini alianza kwa kuweka picha ya gazeti inayowaonesha akiwa na Diamond kwenye habari iliyohusu tamasha hilo na kuandika ‘Hahahaha #DomoSeriously???? Rapper huyo hakuishia hapo aliweka picha nyingine ya Diamond na kuandika: “U talkin money or u talkin nonsense au anashindana na ndovu kun***a? Mwisho alimalizia kwa kujibu tweet ya mtu mmoja aliyemwambia kuwa huyo ni Diamond kwa kuandika: Unfortunately only “diamonds” I know is the ones on ma neck fam.”

DIVA WA CLOUDS FM AJIPIGA TATOO YA KICHINA KIUNONI...

Image
Katika  kile  kinachotafsriwa  kuwa  ni  harakati  za  kulimwagilia  maji  na  marashi  penzi  lake  kwa  prezzo, Diva  wa  clouds fm  sasa  ameamua  kujipiga TATOO YA  KICHINA  kiunoni  ili  kumchanganya  mwanakaka  wa  Kenya  anayegombaniwa  na  warembo  kibao... Diva amejikuta  katika  ugomvi  mkubwa  na  warembo  wa  Kenya  ambao  wanadai  kunyang'anywa   mpenzi  wao.Miongoni  mwa warembo hao  ni Hudahh  aliyekuwa  mshiriki  wa  Big Brother mwaka huu  akiiwakilisha  Kenya... Kabla  ya  kujipiga  tatoo ya  kichina  kiunoni, Diva  aliwahi  kujianika  akiwa  nusu  uchi  huku  shanga  zake  zikiwa  hadharani.  Uamuzi  huo...

MAMA AJIFUNGUA MTOTO ANAYEFANANA NA NYANI.

Image
hatimaye uko nchini NIGERIA   Mwanamke  mmoja  amejikuta  akimwaga  machozi  baada  ya  kumpoteza  mwanaye  dakika  chache  baada  ya  kujifungua.... Tukio  hilo  lilitokea  siku  ya  jumatatu  katika  hospitali  ya Kargo nchini Nigeria...  Taarifa  zinadai  kuwa  mwanamke  huyo  ambaye  ni  mkazi  wa  kijiji  cha  SabonIcel  alijifungua  mtoto wa  ajabu  anayefanana  na  Nyani, hali  iliyomfanya  afariki  dakika  chache  baada  ya  kuzaliwa  Daktari aliyehusika  na  kumsaidia  mwanamke  huyo  anadai  kwamba, mwanamama  huyo  alifikishwa  hospitalini  hapo  majira  ya  saa  moja  na  nusu  asubuhi  na  kwamba  tahadhari ...

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

Image
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.   Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa. Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.     Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela     Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu ...