HIKI NDO KIASI CHA PESA ANACHO INGIZA RAISI OBAMA KWA MWAKA
BAADA ya kuchaguliwa katika awamu ya pili ya utawala wa Marekani, Rais Barack Obama, ameendelea kupata mshahara wa dola 400,000 kwa mwaka.
Wakati alipopata utawala, Rais huyo mwenye nguvu duniani ameendelea kuwa Kamanda wa Jeshi la Marekani, Rais mwenye nguvu duniani na ameendeleza utawala wa Air Force One.
Obama alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza, kipato chake kilikuwa dola 1.3 milioni. Miaka minne baada ya kukaa Ikulu kipato chake kimeongezeka kwa asilimia 800 sasa anapata dola 11.8 milioni.
Kipato kimeongezeka vipi?
Awali Obama alikuwa na kipato kidogo, alikuwa akilipwa dola 60,000 kwa mwaka alipokuwa Seneta wa Illinois na baadaye akawa analipwa dola 175,000 kwa mwaka.
Jambo la kufurahisha ni kuwa kabla Obama hajawa Rais, hakuwa na mshahara mkubwa, hata mke wake, Michelle, alimzidi kwa kipato. Michelle alikuwa akiingiza kiasi cha dola 320,000 kwa mwaka, wakati huo alikuwa Makamu wa Rais wa Kitengo cha Ushirikiano wa Jamii katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Chicago.
Lakini Michelle alipitwa mshahara na mume wake wakati Obama alipounasa urais.
Kipato cha Obama kilianza kukua baada ya kujiimarisha kwenye Chama cha Democratic mwaka 2004.
Vile vile jina la Obama lilikua baada ya kuuza kitabu chake alichokiandaa tangu mwaka 1995 kiitwacho ‘Dreams From My Father’.
Mwaka 2005, kipato cha Obama kiliongezeka kufikia dola 200,000 na hivyo akatimiza dola 1.7 milioni kwa mwaka. Mwaka 2006 kipato cha Obama kilikua na kufikia dola 916,000.
Kitabu cha pili cha Obama kiitwacho ‘Audacity of Hope’ kilitolewa Oktoba, 2006 na kiliongoza kwa mauzo makubwa kiasi cha kumfanya Obama apate dola 4.2 milioni mpaka kufikia mwaka 2007.
Mpaka sasa Obama amekuwa akipata dola 3.75 milioni kutokana na kuuza vitabu vyenye gamba gumu na dola 1.12 milioni kutokana na kuuza vitabu vyenye gamba la kawaida.
Kwa kuwa Obama haruhusiwi kutoa vitabu kuhusu maisha yake ya urais kwa sasa, watu wanasubiri wakati atakapomaliza utawala wake mwaka 2016 ambapo atatoa vitabu vingi zaidi.
Rais George W. Bush, aliwahi kuingiza dola 7 milioni kwa kuandika kitabu cha ‘Decision Points’ na Bill Clinton alipata dola 15 milioni kwa kuandika kitabu cha ‘My Life’.
Lakini ukweli ni kwamba Clinton aliuza vitabu vichache kuliko Bush, kitu kilichomsaidia kupata fedha nyingi ni bei kubwa ya vitabu vyake.
Inakadiriwa kuwa Obama atakuwa amejikusanyia kiasi cha dola milioni 100 au zaidi wakati atakapostaafu kazi. Huenda akafuata nyayo za Bill Clinton ambaye alimaliza utawala wake akiwa na utajiri wa dola 80 milioni.
Historia ya kipato cha familia ya Obama
2000: Dola 240,000
2001: Dola 272,759
2002: Dola 259,394
2003: Dola 238,327
Historia
2005: Dola 1,655,106
2006: Dola 983,826
2007: Dola 4,139,965
2008: Dola 2,656,902
2009: Dola 5,505,409
2010: Dola 1,728,096
2011: Dola 789,674
Jumla: Dola 18,563,000
Historia
Barack Obama ambaye ni rais wa 44 wa Marekani, alizaliwa Honolulu, Hawaii. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Columbia na Chuo Kikuu cha Sheria cha Harvard.
Wakati akisoma sheria, alikuwa pia akifanya kazi za maendeleo ya jamii huko Chicago. Baada ya kumaliza masomo hayo alifanya kazi katika Kitengo cha Haki za Raia huko Chicago na kuanzia 1992 mpaka 2004 alifundisha Sheria ya Katiba katika Chuo Kikuu cha Chicago.
Obama alianza kuonekana mbele za watu wakati alipojiimarisha kwenye Chama cha Democratic mwaka 2004. Novemba 2008 alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani na Januari 2009 aliingia Ikulu.
Obama ni mume wa Michelle, baba wa watoto wawili wa kike, Malia Ann aliyezaliwa mwaka 1998 na Natasha ‘Sasha’ aliyezaliwa mwaka 2001.
Obama ni mume wa Michelle, baba wa watoto wawili wa kike, Malia Ann aliyezaliwa mwaka 1998 na Natasha ‘Sasha’ aliyezaliwa mwaka 2001.
Comments
Post a Comment