MREMBO SUDAN AOLEWA KWA NG’OMBE 520, TOYOTA 3 KALI
Nyalong na mumewe Kok Alat siku ya ndoa.
Mrembo Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka na kila mtu alikuwa tayari kutoa mahali bab’kubwa ikiwa ni pamoja na Sh. milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na Sh. milioni zipatazo 20 za Tanzania!
Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, Nyalong, mrembo wa kabila la Dinka, alikuwa nadhari ya mshangao uliowapata watu waliokuwa katika sherehe hiyo.
Nyalong akiwa nyumbani kwao; na baba na nduguze kabla ya ndoa.
Nyalong, mumewe.
Comments
Post a Comment