Waziri Kabudi akwepa kujibu swali la Zitto Kabwe

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi amekwepa kujibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kutokana na kile alichokisema kuwa ni mtego ambao unaweza kuliingiza taifa kwenye hasara dhidi ya kesi zake za kimataifa.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa 13 Zitto Kabwe amehoji juu kwanini serikali ishitakiwe wakati imekuwa kwenye mazungumzo na kampuni tanzu za ACACIA pamoja na kuhoji kwanini serikali imefungua kesi dhidi ya kampuni za madini juu ya kukwepa kodi.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi akijibu swali amesema maswali ya mbunge huyo asingeweza kuyajibu kwasababu yataathiri ushahidi wa serikali kwenye kesi zake zinazoendelea.

"Masuala yote ya uliyoyasema yaliyo kwenye mahakama za kitaifa na kimataifa ni yanaendelea, nataka niwaambie mtego huo uwe wa bahati mbaya, wa kutumwa au bahati ambaya sitauingia kamwe kwa sababu utaathiri hoja za serikali kwenye kesi zake."

Awali Waziri wa huyo wa Katiba na Sheria alisema katika kesi ambazo serikali inashtakiwa imeshawasilisha ushahidi lakini bado hazijatolewa
hukumu na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na ACACIA kwenye mahakama ya kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog