RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WAHANDISI, ATEMBELEA KIKOSI CHA ANGA MAJUMBA SITA UKONGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya  pamoja na Wanajeshi wa JWTZ Kikosi cha Anga 603 KJ Majumba Sita Ukonga jijini Dar es salaam  alikotembelea kuwapongeza kwa kusherehekea miaka 52 ya Jeshi la Wananchi leo Septemba 1, 2016

Rais Magufuli awataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu

Na Sheila Simba-MAELEZO 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka  wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.

Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.

“mkiamua nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.

Aidha amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.

“Tumemsikia waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili, wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa ndani”Alisema Rais Magufuli

Akimkaribisha rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.

“serikali inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.

Aidha Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.

“Katika kuhakikisha miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda

Comments

Popular posts from this blog