Mwanzilishi wa Facebook Alivyokutana na Akina Yemi Alade Nigeria
Lagos, Nigeria
MWANZILISHI
na mmiliki wa mtandao maarufu duniani wa Facebook, Mark Zuckerberg juzi
Jumanne alianza ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria, ikiwa ni ziara
yake ya kwanza kwa nchi za Afrika, na kukutana watu mbalimbali wakiwemo
wasanii maarufu wa uigizaji filamu na muziki nchini humo.
Katika
ziara hiyo, Zuckerberg aliwasili Lagos Jumanne na kufika kwenye kituo
maarufu cha ubunifu wa masuala ya mitandao ya kijamii cha Yaba,
kilichopo eneo lijulikanalo kam Silicon Valley.
Zuckerberg
alifanikiwa kutoa elimu ya biashara na masoko kwa watu waliohudhuria
kwenye mkutano wake huku akitanua wigo wa watumiaji wa mitandao
anayoimiliki ikiwemo Facebook, Instagram na WhatsApp.Baada
ya somo hilo la juzi Jumanne, Zuckerberg jana aliamkia mitaani asubuhi
akitembelea vijana kwenye Jiji la Lagos bila ulinzi. Alionekana
akikifanya jogging kwenye daraja la Lekki Bridge na vijana. Baadhi
ya wasanii wa filoamu na muziki nchini Nigeria jana ni pamoja na
Richard Mofe Damijo, Kunle Afolayan, Stephanie Okereke Linus, Rita
Dominic, Chidinma Ekile, Yemi Alade na Bright Okocha Basketmouth.
Comments
Post a Comment