Zitto Kabwe afunguka yake kuhusu Oparesheni UKUTA
Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka
maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba.
“Sioni ni kwanini tunahangaika na
vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA
kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache
watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la
kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na
wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini
kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hata hivyo, vikao vya maridhiano
vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa matunda kwenye suala la mgogoro
wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya upinzani wameridhia kurejea Bungeni
katika vikao vitakavyoanza mapema mwezi ujao.
Serikali imeendelea kuwaonya watu wote
wanaopanga kuandamana Septemba 1 huku viongozi wa Chadema wakisisitiza
kuwa siku hiyo watafanya maandamano kama walivyopanga.
Hali hiyo imepelekea kumtoa hadharani
Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ameomba marais wastaafu kumshauri Rais
Magufuli ili kuruhusu Serikali kukaa na Chadema kusaka muafaka wa
masuala ya kisiasa nchini.
Comments
Post a Comment