Mghwira wa ACT-Wazalendo Azindua ‘Tanzania Role Model’
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazarendo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Anna Mghwira, akizindua mashindano hayo.
Mratibu wa mashindano hayo, Samweli Charles (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Mghwira.
Mshereheshaji ‘MC’ wa hafla hiyo, Sufian Juma (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo baada ya shindano kuzinduliwa.
MWENYEKITI wa ACT-Wazalendo na
aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira, jana
alizindua shindano lijulikanalo kama ‘Tanzania Role Model’
lililoandaliwa na kampuni ya Mass Television Company (MTV) chini ya
mkurugenzi wake, Samweli Charles.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli
ya Oceanic Resort iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya
washiriki 17 waliwakilisha hifadhi 17 za mbuga za wanyama hapa nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mratibu
wa mashindano hayo, Samwel Charles, alisema kuwa washiriki watakaa
kambini kwa muda wa miezi mitatu wakitembelea hifadhi za taifa kama
mpango wa kuhamasisha na kukuza utalii wa ndani kupitia warembo hao.
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo,
Anna Mghwira, alisema kuwa nchi hii ina utajiri mkubwa wa asili tatizo
lipo katika kuutangaza, hivyo kwa kupitia mashindano hayo nchi inaweza
kuutangaza utajiri huo hususani kwa kupitia utalii.
Alisema kila mwananchi anayepewa fursa
ya kwenda katika mbuga za hifadhi ahakikishe anakuja na takwimu nzima ya
hifadhi husika juu ya mambo atakayoyaona nakuyawasilisha katika jamii
ili kuyatangaza.
Aidha, washiriki hao wakiwa kambini
wataweza kujifunza mambo mbalimbali kama vile masuala ya mazingira,
afya, vipaji, elimu na mengineyo.
Mghwira aliwataka Watanzania kufuatilia
shindano hilo kwani linahamasisha uhifadhi wa mbuga zetu na akawataka
wafadhili wengine kujitokeza kwani ni moja ya fursa za wao kujitangaza
shughuli zao kibiashara.
NA DENIS MTIMA/ GPL
Comments
Post a Comment