Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inataka Bilioni 864 kwenye bajeti ijayo
May 16 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
imewasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka
2016/2017 pamoja na kuwasilisha maombi ya fedha zaidi ya Bilioni 864.
Hotuba imesomwa na Waziri wake Charles Kitwanga.
Waziri Kitwanga amesema..>>> ‘Wizara
yangu imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya watumishi ndani
ya vyombo Wizara pamoja na wananchi wanaolalamikia utendaji wa vyombo
hivyo’
‘Katika
kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016 Wizara kupitia idara ya
malalamiko 238 yanayohusu utendaji kazi wa vyombo vya kijeshi ndani ya
Wizara kutoka kwa wananchi kupitia njia ya barua, simu, barua pepe,
nukushi pamoja na mahojiano’
‘Ili
kuiwezesha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutekeleza majukumu yake
katika mwaka wa fedha 2016/2017, naliomba Bunge lipitishe makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 ya jumla ya Shilingi 864,106,290,105‘
‘Kati
ya fedha hizo shilingi 316,126,377,000 ni za matumizi mengineyo,
Shilingi 500,056,492,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi
47,923,421,105 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo‘
Comments
Post a Comment