RC PAUL MAKONDA ASEMA WANAWAKE NDIO CHANZO CHA UFISADI NCHINI
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua machinjio ya Vingunguti
baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Dar es Salaam leo
asubuhi. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto.
Wananchi
wa Kata ya Mnyamani Vingunguti wakiwa kwenye mkutano huo wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani)
Makonda (kushoto), akisalimiana na wananchi na viongozi wakati akiwasili kwenye mkutano huo.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia),
akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda kuzungumza na wananchi. Kutoka kulia ni Diwani
wa Kata ya Mnyamani, Shukuru Dege, RC. Makonda na Meneja wa Benki ya
Wananchi Dar es Salaam (DCB), Tawi la Ukonga, Das Ndazi.
Meneja
wa Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB), Tawi la Ukonga, Das Ndazi
(kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu suala zima la utoaji wa
mikopo.
RC Makonda akizungumza na wananchi wa Vingunguti.
Wananchi wakimsikiliza RC Makonda.
Safari ya kwenda kukagua machinjia ya Vingunguti.
Sehemu ya machinjio ya Vingunguti.
RC Makonda akipatiwa maelezo kuhusu mitambo ya kuchinjia iliyopo kwenye machinjio hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni
chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha
za kifisadi.
Makonda
aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani
Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata
mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).
"
Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea
fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa
hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi"
aliseama Makonda.
Makonda
aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia
na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo
jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya
kusafisha miji yetu.
Katika
hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya
Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa
kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia
mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).
"Nimefurahishwa
na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili kujiletea
maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia
jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na
tija" alisema Makonda.
Comments
Post a Comment