Kassimu Majaliwa Akutana na Viongozi Mbalimbali, London Uingereza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda
na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri Mkuu wa
Norway, Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na
rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano
kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa
Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Kulia ni Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Augustine Mahiga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda
na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri
Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia) katika Mkutano kuhusu mikakati
ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House,
London Uingereza, May 12, 2016. Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mohamed Othman na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na
Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa
wa Uingereza (Minister of State for International Development) ,
Justine Greening katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa
uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12,
2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland
katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika
kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.
Comments
Post a Comment