Picha za Waziri wa Sudan Zazua Gumzo Mtandaoni.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini Mh. Mabior Garang De Mabior ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini na kiongozi wa zamani wa kikundi cha waasi cha SPLA/M cha Sudan Dr. John Garang amekuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake zenye utata kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Mabior Garang ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu John Garang ambaye aliongoza kikundi cha waasi kwa muda mrefu kabla ya kufariki katika ajali ya Helkopta mwaka 2005 akiwa Rais wa Sudan Kusini, alifukuzwa katika kikao cha Baraza la mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili.

Mwaka 2014, Mabior aliwahi kukamatwa na maafisa usalama wa Ethiopia kwa kile kilichohisiwa kuwa jaribio la kutaka kumuua Rais wa sasa wa Sudan Kusini Salva Kiir baada ya kukamatwa akiwa hotelini na bastola ikiwa na risasi sita. Baada ya kukamatwa na kuhojiwa alisema alitaka kukutana na Rais Kiir kwani ameharibu kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Baba yake John Garang.

Mabior Garang anahudumu katika Serikali ya Umoja kupitia Dr Riek Machar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusin

Comments

Popular posts from this blog