WAKUU WA SHIRIKA LA KUPAMBANA NA UFISADI NCHINI KENYA WASIMAMISHWA KAZI
Rais wa
Kenya, Uhuru Kenyatta, amewasimamisha kazi wakuu wawili wa shirika
linalopambana na ufisadi nchini humo, siku moja tu baada ya bunge
kupitisha mswaada inaowalaumu kwa uzembe na utepetevu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu,
tume ya maadili na kupambana na ufisadi, itaendelea na kazi yake licha
ya kusimamishwa kwa wakuu hao wawili.
Wakuu hao ambao ni Mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi. Irene Keino wamesimamishwa huku
uchungunzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za uzembe wa kazi
na kutumia vibaya madaraka yao ikiwemo kujihusisha na ufisadi.
Tangazo
hilo limetolewa mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka ya tume hiyo
kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta, ripoti iliyosababisha kusimamishwa kazi
kwa Mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na Maafisa wengine 12
na Wakuu serikalini ili kupisha uchunguzi ufanyike dhidi yao
Comments
Post a Comment